Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 09.14.2017

  • WATU WAWILI (02) WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE WATANO (5) KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI ILIYOTOKEA WILAYANI KWIMBA.

KWAMBA TAREHE 13.09.2017 MAJIRA YA SAA 16:10HRS KATIKA BARABARA YA NYASAMBA – SHILIMA KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA SHILIMA KATA YA KIKUBIJI WILAYA YA KWIMBA  MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T.794 AMT MITSUBISHI CANTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DAREVA AITWAYE BALELE MIPAWA MIAKA 28, LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO KWA WATU WAWILI AMBAO NI 1.ALANI NKALANGO MIAKA 29, MKAZI WA KIJIJI CHA NYASAMBA NA 2.CHARLES PASTORY MIAKA 45, MKAZI WA KIJIJI CHA NYASAMBA NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA WATU WENNGINE WATANO AMBAO NI 1.ROBERT DAKTA, MIAKA 26, 2.MALANDO JOSEPHAT, MIAKA 30, 3.PAUL JAMES, MIAKA 17, 4.MWAZALIMA SALU, MIAKA 17, NA 5.JUMA NKALANGO, MIAKA 44, WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA NYASAMBA KILICHOPO WILAYANI KISHAPU MKOANI  SHINYANGA.
INADAIWA KUWA GARI LILIKUWA LIMEBEBA WACHEZAJI MPIRA WALIOKUA WAKITOKEA KIJIJI CHA NYASAMBA KILICHOPO WILAYA YA KISHAPU MKOA WA SHINYANGA KWENDA KUCHEZA MPIRA KATIKA KIJIJI CHA KIKUBIJI KILICHOPO WILAYA YA KWIMBA MKOANI MWANZA. INASEMEKANA KUWA DEREVA WA GARI HILO ALIPITIA NJIA YA VUMBI HUKU AKIWA KWENYE MWENDO KASI ILI WAWEZE KUFIKA MAPEMA WACHEZE MPIRA. INADAIWA KUWA GARI LILIKUWA LIMEBEBA WACHEZAJI MPIRA NA BAADHI YA MASHABIKI, GARI HILO LILIACHA NJIA BAADA YA DEREVA KUSHINDWA KULIMUDU NA BAADAE KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI NA MAJERUHI TAJWA HAPO JUU.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA WA GARI AMEKATWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI. MAJERUHI WOTE WATANO WANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KWIMBA NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI, MIILI YA MAREHEMU PIA IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA KWIMBA KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ITAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO AKIWATAKA KUTII SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI BILA SHURUTI ILI KUEPUSHA MAJERUHI NA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA PIA ANAWATAKA ABIRIA HUSUSANI VIJANA WACHEZA MPIRA KUACHA ULIMBUKENI WA KUSHINDWA KUMUONYA DEREVA PINDI ANAPOENDESHA GARI KINYUME NA UTARATIBU KWANI WANAJIHATARISHIA MAISHA YAO.
IMETOLEWA NA:
DCP; AHMED MSANGI.
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

No comments