Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 07.09.2017
  • MWANAMKE MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMFANYIA UKATILI MTOTO WA KUMCHOMA MOTO MDOMO BAADA YA KUDOKOA MBOGA JIKONI WILAYANI NYAMAGANA.

KWAMBA TAREHE 06.09.2017 MAJIRA YA SAA 09:15HRS ASUBUHI KATIKA MTAA WA LOROTE – NYAKATO WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, VICTORIA WILLIAM MIAKA 25, MKAZI WA LORETO – NYAKATO, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMFANYIA UKATILI WA KUMCHOMA MOTO MDOMO MTOTO AMBAYE NI SHANGAZI YAKE AITWAYE MARTHA MICHAEL MIAKA 07, MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA SHULE YA MSINGI SIMA, HII NI BAADA YA KUDOKOA MBOGA JIKONI, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIWAOMBA WAZAZI WA MTOTO KWAMBA WAMGAIE MTOTO AJE KUISHI NAE  HUKU MWANZA ILI AMLEE. INASEMEKANA KUWA BAADA YA KUELEWANA MTUHUMIWA ALIKUJA NA MTOTO HUKU MWANZA NA KUANZA KUISHI NAE HAPO NYUMBANI KWAKE.
INADAIWA KUWA MAJIRA YA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAJIRANI WALISIKIA MTOTO AKIPIGA YOWE AKIOMBA  MSAADA, NDIPO WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUMKUTA MTOTO AKIWA ANACHOMWA MOTO MDOMONI NA SHANGAZI YAKE BAADA YA KUTENDA KOSA LA KUDOKOA MBOGA JIKONI. WANANCHI BAADA YA KUONA TUKIO HILO WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA USTAWI WA JAMII HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA.
POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MAJERUHI AMEPELEKWA HOSPITALI KUPATIWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA RAI KWA WAZAZI NA WALEZI AKIWAOMBA WAWALEE WATOTO KATIKA MAADILI MAZURI NA KUACHA TABIA YA KUWAPA ADHABU MBAYA PINDI WANAPOKOSEA ZINAZOWEZA KUGHARIMU MAISHA YA WATOTO, KWANI ADHABU ZA AINA KAMA HIYO NI KOSA KISHERIA NA ZINAWEZA KUPELEKEA MZAZI/MLEZI KUFUNGWA NA BAADAE WATOTO KUKOSA MTU WA KUWALEA. PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI LIWEZE KUDHIBITI UHALIFU KATIKA MKOA WETU.


IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI.
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

No comments