Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA


msangii-1
TAREHE 22.09.2017 MAJIRA YA SAA 20:00HRS USIKU KATIKA KIZUIZI CHA TRA KILICHOPO BARABARA YA MWANZA KWENDA MUSOMA KATA YA ITUMBILI WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. JAMES LAWRENCE, MIAKA 51, MKAZI WA TARIME – MARA, AMEKAMATWA AKIWA NA MIRUNGI KIASI CHA KILO 35, ALIYOKUWA AKISAFIRISHA TOKA SIRALI KUJA MWANZA KWENYE BUS LENYE NAMBA T.498 DAK, AINA YA YOUTONG, MALI YA KAMPUNI YA GEORGE TOWN, NA 2.MAGABE MIRUMBE MIAKA 45, MKAZI WA TARIME –MARA, AMEKAMATWA AKIWA NA MIRUNGI KIASI CHA KILO 09, ALIYOKUWA AKISAFIRISHA TOKA SIRALI KUJA MWANZA KWENYE BUS LENYE NAMBA T. 201 DAN AINA YA YOUTONG, MALI YA KAMPUNI YA ZAKARIA, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

AWALI ASKARI WALIKUWA KWENYE KIZUIZI TAJWA HAPO JUU WAKISIMAMISHA NA KUPEKUA MAGARI YOTE YALIYOKUWA YAKIPITA KWENYE BARABARA YA MWANZA KWENDA MUSOMA, ILI KUWEZA KUBAINI MADEREVA NA ABIRIA WANAOSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA. AIDHA WAKATI WAKIENDELEA KUSIMAMISHA NA KUPEKUA MAGARI HAYO WALIWEZA KUKAMATA MAGARI TAJWA HAPO JUU YAKIWA NA ABIRIA HAO WALIOKUWA WAKISAFIRISHA MIRUNGI KIASI CHA KILO 44 TOKA SIRALI –TARIME KUJA MWANZA.
POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE WAWILI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WAWILI WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA MSAKO WA KUWATAFUTA NA KUWAKAMATA WAUZAJI, WASARISHAJI NA WATUMIAJI WENGINE WA MADAWA YA KULEVYA BADO UNAENDELEA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MKOA WA MWANZA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WOTE WA JIJI NA MKOA WA MWANZA NA WAMAENEO YA MIKOA YA JIRANI AKIWATAKA KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA KWANI NI KOSA LA JINAI, BALI WANANCHI WAFANYE KAZI HALALI YA KUJIPATIA KIPATO NA WALA SIO VINGINEVYO. AIDHA PIA ANATOA RAIA KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA MABASI KUACHA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA KWANI KOSA KISHERIA.
 IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

No comments