Header Ads

Responsive Ads Here

SUMATRA PWANI YASISITIZA NAULI MBEZI -KIBAHA NI SH.500/MBEZI-MLANDIZI SH.1,600


IMG-20170926-WA0020
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MAMLAKA ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA),mkoani Pwani ,imewaasa wamiliki wa mabasi madogo ya abiria(daladala) yanayofanya safari zake Mbezi -Kibaha kuacha kupandisha nauli tofauti na zilizotangazwa kisheria.

Imesisitiza nauli halali kutoka mbezi hadi Kibaha ni 500 badala ya 800 wanayoitoza kwa sasa kwa abiria na Mbezi-Mlandizi ni sh.1,600 badala ya 1,800/2,000 inayolipishwa.
Aidha kuanzia sasa basi litakalobainika kutoza nauli tofauti na elekezi atafikishwa mahakamani ama kutozwa faini.
Hayo aliyasema na ofisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA)mkoani Pwani, Omary Ayubu,mjini Kibaha baada ya kufanya zoezi la kushtukiza kukamata magari yenye makosa mbalimbali,kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani hapo kupitia kitengo cha usalama barabarani.
Alisema wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kutoka kwa abiria kuwa wanatozwa nauli kubwa suala amabalo ni kinyume na sheria.
Ayubu alitaja viwango vya nauli vinazopaswa kulipwa kuwa ni Mbezi- Kiluvya kwa Komba sh.400 badala ya sh.700 na Mbezi-Picha ya Ndege sh.700 badala ya 900.
Maeneo mengine ni Mbezi hadi Mlandizi sh.1,600 badala ya 1,800/2,000, Mbezi- Kongowe sh.1,100, Mbezi-Vigwaza 2,100, Mbezi-Chalinze 3,200, Mbezi-Lugoba 4,100 na Mbezi-Msata 4,600 .
“Leo katika operesheni hii tumekamata magari 21 kutokana na makosa ya kutokuwa na ticket na kutoza nauli kubwa “
“Madereva nane watapelekwa mahakamani kutokana na kuzidisha nauli kinyume cha sheria na tunawataka wamiliki kuzingatia masharti ya leseni,” alisema Ayubu.

Alisema wataendelea kuwachukulia hatua za kisheria madereva wanaokiuka sheria na ameshukuru wananchi kwa ushirikiano wao wa kutoa taarifa juu ya magari yanayoendelea kutoza nauli ambazo ni kinyume cha utaratibu.
Ayubu aliwataka madereva kuwa na katabia ka kugomo kwani haina faida na badala yake mwenye malalamiko aende ofisini na kuandika barua ndani ya mwezi mmoja ili malalamiko yao yaweze kutafutiwa ufumbuzi.
Nae kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Pwani,Salum Morimori alisema kuwa walifanya ukaguzi kwenye mabasi hayo ili kuangalia ubora wa magari .
Alieleza kumekuwa na malalamiko toka kwa abiria kutopewa tiketi, abiria kuchanganywa na mizigo ,ubovu wa magari,matairi mabovu na kuchakaa kwa viti kwenye magari hayo.
Morimori alisema ,hadi sasa magari 35 yamekamatwa ,kati yake 21 ni makosa yanayosimamiwa na SUMATRA na 14 ni ya kiusalama barabarani.
“Tumefanya zoezi hili la kusthtukiza kwa kushirikiana na wenzetu SUMATRA ili kuwajengea kumbukumbu madereva kufuata sheria za usalama barabarani,” alisema Morimori.
Hata hivyo, alisema kuwa lengo ni kuhakikisha usalama wa wanajamii hasa wanaotumia vyombo vya moto wabaki salama.
“Wamiliki na madereva wahakikishe wanaboresha vyombo vyao viko salama kwa kufanya marekebisho hasa mipira na tunahitaji wanajamii kushirikiana nasi ili kukabiliana na madereva ambao wanakiuka sheria za usalama barabarani” alisema Morimori.

No comments