Header Ads

Responsive Ads Here

SUMATRA MKOANI PWANI YAFANIKIWA KUMALIZA NA KUSULUHISHA SAKATA LA MGOMO WA MADEREVA WA MABASI MADOGO YA ABIRIA


daladala
NA VICTOR MASANGU, PWANI
UONGOZI wa mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi kavu na majini (SUMATRA) Mkoa wa Pwani hatimaye umefanikiwa kumaliza na  kusuluhisha sakata la mgomo uliofanyika jana kwa  madereva wa mabasi madogo ya daladala yanayofanya safari zake kuanzia katika stendi ya mbezi kuelekea  katika maeneo mbali mbali ya Wilayani Kibaha  hadi Msata Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari  kuhusina na sakata hilo mara baada ya kumalizika kwa kikao maalumu baina yao na uongozi wa madereva wa mabasi madogo  Afisa mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Pwani Omary Ayoub amesema kuwa mgomo huo  ambao ulitokea siku ya jana ulidumu kwa kipindi cha zaidi ya masaa saba na kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria waliokuwa wanahitaji huduma ya usafiri.
Ayoub alibainisha  kwamba  wameweza kubaini kuwepo kwa ongezeko la nauli kiholela kwa abiria hao baada ya kufanya zoezi la kugagua magari zaidi ya 100 na kukuta abiria wanalipishwa kiwango kikubwa kinyume kabisa na taratibu,na kuongeza suala hilo kwa sasa wameshakutana na viongozi wa mabasi hayo na kukubaliana kiwango  halali ambacho kinatakiwa kutumika.
“Ni kweli kulikuwa na hali ya sintofahamu baada ya baadhi ya madereva wa mabasi madogo ya abiria yanayoanzia luti zake katika kituo cha mbezi Jijini Dar es Salaam kuelekea maeneo ya Kibaha mpaka msata kugoma kupakia abiria kutokana na kugomea nauli ambayo imepagwa na ipo kihalali kabisa ila kwa sasa nashukuru tumekaa na viongozi wao wa mabasi na tumeshalimaza na viwango vyetu tulivyovipanga ndi vitatumika na sio vinginevyo,”alisema Ayoub.
Ayoub alifafanua zaidi kuhusina na tukio hilo alisema kuwa madereva hao waliamua kugomea kwa makusudi viwango vya nauli kilichopangwa na mamlaka hiyo na kujiamulia kujipangia bei yao mwenyewe na kuwatoza abiria wanaotokea mbezi kuelekea Kibaha  kiwango kikubwa tofauti na kile ambacho kilitolewa hapo awali kitu ambacho ni kinyume kabisa na taratibu.
“Huu mgomo sisi kama Sumatra kwa kushirikiana na jesho la polis tulifanya zoezi la kukagua magari kwa lengo la kuboresha huduma ya usafiri na ndipo  tulipobaini kuna makosa ambayo yanafanywa ya kuwatoza nauli kubwa abiria tofauti na umbali wanayokwenda, na kitu kikubw amfano nauli ya kutokea mbezi kwenda maili moja kibaha inatakiwa kulipia shilingi mia tano lakini cha kushangaza wao walikuwa wanalipisha shilingi mia nane yani wamepandisha mia tatu nzima,”alisema.
Kwa upande wake  Jaheka Mdami  Mwenyekiti wa madereva wa mabasi madogo yanaofanya safari zake kutokea kituo cha Mbezi Jijini Dar es Salaa kuelekea Kibaha amesema kwamba kwa sasa mgomo huo wa madereva  umeshamalizika ambapo wameshakubaliana na uongozi wa Sumatra kutumia viwango vya nauli ambavyo vimeelekwezwa kwa mujibu wa sheria.
Naye Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Pwani Salum Molimoli amesema kuwa wameamua kufanya oparesheni kwa ajili ya kukagua magari mabovu kwa lengo la kuweza kupunguza wimbi la ajali pamoja na kutoa elimu kwa madereva kuhusiana na madhara yatokanaayo na unywaji wa pombe wakati wakiendesha vyombo za moto .
Kamanda Molimoli alisema kwamba kwa sasa wana mikakati kabambe ya kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara ambao utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia ajali za barabarani ambazo wakati mwingine zinatokana na uzembe wa madereva wenyewe.
“Katika kuhakikisha kwamba ajali za barabarani katika Mkoa wetu wa Pwani zinapungua kabisa tumejipanfa kufanya ugaguzi wa mara kwa mara ili kuweza kubaini magari ambayo ni mabovu na yanatembea barabarani, na kitu kingine ni kuweka mipango ya kuweza kutoe elimu zaidi ambayo iataweza kuwasaidia madereva pindi wanapokuwa njiani,”alisema Molimoli.
Mamlaka ua Udhibiti wa Usafiri wa  nchi kavu na majini (SUMATRA)  kwa  kushirikiana na jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefanikiwa  kuyakamata magari zaidi ya 100 kutokana na makosa mbali mbali ikiwemo kuvunja sheria ya kutozingatia sheria za barabarani,kutokufunga mikanda,kuendesha magari mabovu pamoja na  kuzidisha kiwango cha nauli kwa abiria.

No comments