Header Ads

Responsive Ads Here

STAND UNITED YAZINDUKA LIGI KUU YA VODACOM


HMB_8262
Baada ya kuchezea vichapo mechi tatu mfululizo hatimaye Chama la Wana ‘Stand United’ imepata ushindi wa kwanza dhidi ya wagonga nyundo Mbeya City kwa jumla ya  mabao 2-1 Mchezo uliopigwa katika dimba la CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa timu zote mbili ambazo zilipelekea kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana hata bao moja.

Adam Salamba alikuwa wa kwanza kuwanyanyua mashabiki wa Stand United kwa kufunga bao la kuongoza hata hivyo Mohammed Samatta aliisawazishia Mbeya City na kuwanyamanzisha mashabiki wa wapiga debe wa Stand ya Shinyanga.
Baada ya kusawazisha Mbeya City walicheza Mpira kwa kuonana na kuwafanya Stand kucheza kwa kauta na katika dakika ya 62 Ally Ally aliifungia Stand United bao la pili na la ushindi.
Hata hivyo Stand walipata pigo baada ya Nahodha wao Erick Mlilo kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kucheza madhambi hadi mwamuzi anamaliza Mpira Stand wameondoka na ushindi wa mabao 2-1 na kuchukuwa pointi tatu muhimu msimu huu tangu Lingi ya Vodacom ianze.
Stand United mwishoni wa wiki ya Septemba 29 watashuka tena kwenye dimba lao kumenyana na wekundu wa Msimbazi Simba ambao wapo kanda ya Ziwa ya Ziwa na tayari wamecheza mechi moja dhidi ya Mbao FC na kutoka sare ya 2-2.

No comments