Header Ads

Responsive Ads Here

SINGIDA UNITED YAIBUGIZA KAGERA SUGAR ‘MTIBWA SUGAR YAPUNGUZWA KASI LIGI KUU VODACOM


DSC6999
Timu ya Singinda United imeendeleza kugawa dozi katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma baada ya kitandika Kagera Sugar bao 1-0 Mchezo wa Ligi Kuu na ukiwa ushindi wa tatu kwa matajiri hao walio chini ya Kocha mwenye uzoefu na Soka la Tanzania na Afrika Hans Van Der Pluijm.

Kipindi cha kwanza kilikuwa cha mashambulizi kwa timu zote mbili hata hivyo Singida walipata bao huku wakiwa wanashangilia Mwamuzi alikataa bao hilo ambalo liliwachanganya mashabiki na kujiuliza kwanini nilikataliwa hadi mapumziko timu hizo zilikwenda bila kufungana.
Singida United waliingia kipindi cha pili kwa kuliandama lango la Kagera Sugar na kama washambuliaji wangekuwa makini wangeweza kuondoka na ushindi wa magoli mengi na katika dakika ya 87 Mshambuliaji hatari toka Zimbabwe ,Tafadzwa Kutinyu aliwanyanyua mashabiki kwa kufunga bao kwa njia ya mkwaju wa Penalti na kumuacha Kaseja akiwa hana la kufanya.
Kwa Matokeo hayo Singida United wamefikisha jumla ya Pointi 9 na kupanda hadi nafasi ya tatu huku Kagera Sugar wakishuka hadi nafasi ya mwisho ya msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na alama moja .
MTIBWA SUGAR
Katika uwanja wa Mbatini,Mlandizi Mkoani Pwani timu ya Mtibwa  Sugar imepunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting ama unaweza kuwaita wazee wa wiki.
Matokeo haya, yanawafanya Mtibwa ifikishe pointi 10 baada ya kucheza mechi nne, lakini haindoki kileleni hata baada ya mecho zote za Raundi hii ya nne, kwani timu zinazofuatia zina pointi nane kila moja.
Katika mchezo wa leo, bao la Ruvu Shooting lilifungwa na Zuberi Dabi dakika ya kwanza tu, kabla ya Mtibwa Sugar kusawazisha dakika ya 55 kupitia kwa Stahmil Mbonde.

No comments