Header Ads

Responsive Ads Here

SHAHIDI AIELEZA MAHAKAMA JINSI DC ALIVYOPEKUWA CHUMBA CHAKE


Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog
SHAHIDI wa
utetezi katika kesi ya kughushi Mukhtasari,wa serikali ya mtaa wa Levolosi ,mfanyabiashara
,Mathew Moleli ameieleza mahakama jinsi mkuu wa wilaya mstaafu  alivyoingia kwa mabavu nyumbani kwake na
kuamrisha askari polisi aliokuwa ameambatana nao wapekuwe chumba chake
wakitafuta hati inayodaiwa kughushiwa.
 
Akitoa utetezi  mbele ya hakimu Gwanta Mwankuga
wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha ,anayesikiliza shauri hilo huku akiongozwa na wakili wa utetezi Ephraim Koisenge, aliieleza mahakama hiyo jinsi alivyofedheheshwa wakati askari hao,akiwemo mwendesha bodaboda na mlalamikaji Makanga walivyopekuwa chumba chake wakitafuta hati ambayo ni mali.
 
Shahidi huyo aliiendelea kueleza kuwa, mnamo oktoba ,2 mwaka 2014 alishtakiwa katika mahakama ya wilaya iliyopo Sekei mkoani Arusha, kwa shauri kama hilo huku mlalamikaji akiwa ni Danny Makanga na baadae oktoba 1,mwaka 2015 kesi hiyo ilifutwa baada ya upande wa jamhuri kuomba kuondoa shauri hilo mahakamani  jambo ambalo anadai linampotezea muda wake.
 
Alidai kuwa kufutwa kwa shauri hilo aliandika
barua kwa mkuu wa upelelezi wa mkoa wa ARUSHA (RCO) kuomba kurejeshewa  hati yake ya nyumba iliyokuwa inashikiliwa
ofisi ya RCO, jambo ambalo hakuwahi kujibiwa hadi oktoba ,28 mwaka 2016
alipokamatwa na polisi na kufikishwa  mahakamani
akishtakiwa kwa makosa mawili  ya kughushi Mukhtasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi na kuwasilisha nyaraka za kughushi katika ofisi za jiji la Arusha ,
 
Hata hiyo upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali Mary Lucas ulimtaka mshtakiwa kueleza uhalali wa eneo anakoishi kwa sasa ,jambo ambalo shahidi huyo alisema ni mali yake na waliuziana kindugu na mlalamikaji Makanga  bila kuandikishana na baadae alifuata taratibu
zote za kuomba hati miliki kupitika kikao cha dharura kwa uongozi wa serikali
ya mtaa wa Levolosi kilichoketi Septemba,10 mwaka 2006.
 
Pia shahidi huyo alieleza kuwa tangu kikao hicho cha serikali ya mtaa kiketi kwa dharura na baadae kupeleke maombi ya kupatiwa hati ya umiliki wa nyumba yake kiwanja namba 231 kitalu DD kilichopo Mianziani jijini Arusha ,hakuwahi kupata malalamiko yoyote kuhusu kughushi nyaraka za serikali,jambo ambalo ameiomba mahakama
kuifuta kesi hiyo kwa sababu malalamiko hayo hayana ukweli wowote.
 
Kesi hiyo namba 430 ya mwaka 2016 inatarajiwa kuendelea tena ,Septemba 28 mwaka huu ,ambapo upande wa utetezi unatarajia kufunga utetezi wake kwa shahidi wa pili na wa mwisho baada yashahidi wa kwanza ambaye ni mshtakiwa kukamilisha utetezi,ambaye pia aliwasilisha  nyaraka mbalimbali kama vielelezo mahakamani hapo.
 
Awali wakili wa serikali Mary Lucasi alipinga kuwasilishwa kwa baadhi ya nyaraka muhimu za mshtakiwa mahakamani hapo kwa madai kuwa nyaraka  hiyo ni kivuli ,jambo ambalo lilipigwa na wakili wa utetezi Koisenge ambaye aliiomba mahakama izipokee kama kilelezo,jambo
ambalo hakimu Mwankuga baada ya kuzipitia hoja ya upande wa mashtaka aliona hazina mashiko na kuzipokea ili zitumikea mahakamani hapo kama kielelezo.

No comments