Header Ads

Responsive Ads Here

SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO


PMO_0045
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza kabla ya kuzindua  Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.

PMO_0042
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) na Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia kwake) wakishangilia baada ya Waziri Mkuu Kuzindua  Mpango Mkakati Jumuishi wa kitaifa wa Lishe kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.  Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Selemani Jaffo na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde.
PMO_0056
Baadhi ya Washiriki wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
PMO_0079
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango  nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe  baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba  6, 2017.  Kulia kwake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  na kushoto  ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas.
PMO_0094
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya kuzindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
PMO_0110
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango(kushoto kwake) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia kwake) wakionyesha vitabu vya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas
PMO_0136
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katia Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe uliofanywa na Waziri Mkuu,  kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
………………………………

SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 11 ili kukabiliana na utapiamlo na amemtaka kila mdau wa lishe aonyeshe bayana mchango wake katika kukabiliana na utapiamlo nchini.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Septemba 6, 2017) wakati akifungua mkutano wa nne wa mwaka wa wadau wa lishe wa kutathmini afua za lishe nchini kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. Pia alizindua Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe wa mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 (Joint Multisectoral Nutrition Review).
“Viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali wabaini kiwango cha utapiamlo katika maeneo yao, waonyeshe mbinu za kukabiliana na hali hiyo, wafanye tathmini ya ufanisi na watoe taarifa za ufanisi,” amesema.
Amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote, wahakikishe shilingi 1,000 ambazo Halmashauri zilielekezwa kutenga kwenye bajeti kutoka kwenye vyanzo vyao vya mapato kwa ajili ya kuboresha lishe kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano, zinatolewa na kutumika kama ilivyopangwa.
“Tulikubaliana kila Halmashauri lazima ikusanye makusanyo ya ndani kwa asilimia zaidi ya 80. Nilisema kiwango cha chini kisipungue asilimia 80. Na kupitia makusanyo hayo, ndipo tunapata fedha za kutenga kwa masula kama haya,” alisisitiza.
“Napenda kusisitiza kwamba ni lazima tufanye tathmini ya wapi tumefikia na wapi tumekwama katika kupambana na tatizo la utapiamlo hapa nchini,” alisema.
Pia amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wahakikishe wanaisimamia mikoa na halmashauri zao kutekeleza afua zilizoainishwa katika Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe kwa kuzijumuisha katika mipango yao na kuzitengea fedha kwenye bajeti zao za kila mwaka. 
Wakati huohuo, Waziri Mkuu alisema amefurahishwa sana na kaulimbiu ya mkutano huo isemayo “Lishe Bora: Msingi wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania” ambayo kimsingi inaendana na dhamira yetu ya kujenga uchumi wa viwanda kama kichocheo cha mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.
Pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wadau wawekeze kwenye viwanda vya usindikaji wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi ili kuongeza wingi wa vitamini na madini katika vyakula na hatimaye kuboresha lishe na afya ya jamii. “Napenda kusisitiza kuwa Serikali imeandaa mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo tutumie fursa hii kikamilifu,” aliongeza.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu alisema kuna baadhi ya Halmashauri na mikoa hazijaunda Kamati za Afua za Lishe.
“Ninaomba Halmashauri na mikoa ikamilishe kuunda kamati za mikoa na pia watendaji wahakikishe fedha zimetengwa na zinatolewa. Lakini cha msingi ni kwamba fedha hizi zitumike kwa matibabu ya utapiamlo na masuala ya lishe na si vinginevyo,” alisisitiza.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
  1. L. P. 980,
40480 DODOMA, 
ALHAMISI, SEPTEMBA 7, 2017.

No comments