Header Ads

Responsive Ads Here

SERIKALI YATAKIWA KUSIKILIZA SAUTI ZA WATOTO KUFANIKISHA MALENGO ENDELEVU UN


taifa
Na Mahmoud Ahmad, Arusha
Wadau wa masuala ya watoto Pamoja na Serikali wametakiwa kuhakikisha wanasikiliza sauti za watoto wanazopaza katika kuhakikisha malengo endelevu ya umoja wa mataifa yanafanikiwa ilikuweza kuwasaidia na kufikia malengo yao ikiwemo changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo na kuzipatia majibu kwa wakati wakitunga sera.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kijamii inayoshughulikia masuala ya watoto(REPSSI) Edwick Mapalala wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa watoto kutoka mataifa 13 ya Afrika mashariki na kusini mwa Afrika unaoendelea jijini Hapa.
Mapalala Alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kusikiliza masuala mbali mbali yanayowagusa watoto kutoka kwenye jamii yakiwemo malengo matano ya umoja wa mataifa kuhusu haki za motto, na kupata kutoka kwa wahusika na kuweza kusikiliza wanayokumbana nayo kwenye jamii ilikuweza kuwa na sera nzuri za kuwasaidia katika makuzi yao.
Amesema kuwa jamii imekumbwa na wimbi la unyanyasaji watoto ikiwemo kufanyishwa kazi na kunyimwa haki yao ya kusoma na wengine hata kuwafungia majumbani na kukosa stahiki zao hivyo watoto hawa ni sehemu ya kujua changamoto wanazokumbana nazo ili tuweze kuzijadili na mwisho wa siku kuondokana na unyanyasaji.
“Mkutano huu una lengo la kuja na majibu na njia za kuwasaidia watoto katika ukuaji wao hadi wanapofikia watu wazima ndio maana tumewaalika wao ilikusikiliza changamoto wanazoziona katika jamii ilikuweza kupata sauti yao kwa umoja wetu”alisema Mapalala.
Wakati huo huo akifungua mkutano huo Katibu mkuu wa wizara ya Afya Dkta Ulisubi amesema kuwa malengo endelevu ya millennium yameweka wazi jinsi ya kuwasaidia watoto kwenye changamoto za kielimu,Afya na wao kama serikali wanatambua jukumu lao la kuhakikisha watoto wanapata huduma bora ikiwemo zile za msingi ili kuwa na taifa lenye watu waliokamilika siku za usoni.
Amesema kuwa suala la changamoto wanazokumbana nazo watoto hapa nchini limekuwa likipewa kipaumbele na serikali yetu katika kuhakikisha tunakuwa na watu watakaoweza kulijenga taifa letu wakiwa na ustawi na Afya bora  sanjari na kufuata maadili ndio maana wizara imekuwa mstari wa mbele kuliangalia hilo.
Dkta Ulisubi alisema kuwa Nchi yetu imekuwa na mipango mbali mbali inayowagusa watoto wetu na kuweza kuwasaidia ikiwemo masuala ya Afya ya jamii na kinga kwa watoto katika maradhi mipango ya lishe mashuleni na mengine yote ikiwa ni kuisaidia jamii ya watoto kuweza kufikia malengo yao.
Mkutano huo utaenda sambamba na mkutano utakoanza 4-6 utakaowakutanisha wadau wa watoto,serikali na mashirika yanaosimamia haki za watoto kutoka mataifa hayo lengo likiwa ni kujadili na kuzisikia sauti zilizopazwa na watoto kutoka kingo za bara hili.

No comments