Header Ads

Responsive Ads Here

SERIKALI YARIDHISHWA NA WELEDI NA UTENDAJI KAZI WA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII KATIKA KUHUDUMIA WANANCHI WANYONGE.


Pix 1
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Dodoma katika kikao kilichofanyika ukumbi wa manispaa ya Dodoma, tarehe 16 Sept, 2107.

Pix 2
Mratibu wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Mwajina Lipinga (kulia) akifafanua masuala mbalimbali kuhusu utendaji kazi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhusu uratibu wa majukumu ya Maendeleo ya Jamii nchini kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Dodoma katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa manispaa ya Dodoma.
Pix 3
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Atupele Mwambene akizungumzia masuala mbalimbali ya Kisera  kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Dodoma katika kikao kati ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii na  Maafisa Maendeleo ya jamii wa mkoa wa Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Dodoma.
Pix 4
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini(HGCU) Bw. Erasto Ching’oro(kulia) akitoa maelezo ya upatikanaji wa Sera na machapisho mbalimbali zinazohusu masuala ya Maendeleo ya Jamii kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Dodoma katika kikao baina ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii na  Maafisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Dodoma kilichofanyika kwenye ukumbi wa manispaa ya Dodoma. 
Pix 5
Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya ya Bahi Bw. Mchapa Edward akiomba ufafanuzi kuhusu masuala ya kiutendaji katika kikao kati ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii na  Maafisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Dodoma.
Pix 6
Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya ya Mpwapwa Bw. Njovu Mikidadi akitoa maoni  kuhusu masuala ya kiutendaji katika kikao kati ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii na  Maafisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Dodoma.
Pix 7
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka wilaya ya Chamwino Bi. Sophia Swai akitoa maoni yake katika kikao kati ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii na  Maafisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Dodoma.
Pix 8
Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya ya Chemba Bi. Flora Shija akitoa maoni yake katika kikao kati ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Maendeleo yaJamii wa mkoa wa Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Dodoma.
Pix 9
Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka mkoa wa Dodoma wakimsikiliza  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike(hayupo Pichani) wakati wa kikao cha kujadili masuala ya sekta ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Dodoma.
Pix 10
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Mratibu wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wakuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma mara baada ya kikao cha kuhamsha ari ya kushiriki kazi za maendeleo katika kikao kilichojumuisha Maafisa hao kwenye ukumbi wa manispaa ya Dodoma. 
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
……………………………………………………………………………
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amewapongeza maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kwa ujumla kwa kazi wanazofanya kwa ajili ya jamii katika kuamsha ari kwa wananchi katika kujileta maendeleo.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika kikao cha kujadiliana masuala mbalimbali yahusuyo maendeleo ya jamii nchini.
“Niwashukuru sana maafisa Maendeleo ya Jamii kwa kazi nzuri wanazofanya katika jamii hasa katika kuamsha ari ya wananchi kujitolea katika kujiletea maendeleo” alisema Bw. Golwike.
Ameongeza kuwa suala la maendeleo ni la kila mmoja katika jamii na kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii kusaidia katika kuamsha ari zaidi ya wananchi kujitolea katika kujiletea maendeleo.
Kwa upande wake Mratibu wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Mwajina Lipinga amesema kuwa bado kuna fursa ya kufanya zaidi ya wanachokifanya kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii katika maendeleo yao ya kazi.
“Bado tunahitaji kujituma zaidi katika kazi, tufanye kazi na kutimiza majukumu yetu ya kazi kama Maafisa Maendeleo ya Jamii” alisema Bibi. Mwajina.
Ameongeza kuwa ni muhimu kwa Maafisa Maendeleo ya jamii kutekeleza majukumu yao haswa kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Jamii.
Naye kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Atupele Mwambene amesema kuwa Wizara inayafuatilia na kuyafanyia kazi masuala yote ya Sera yahusuyo Maendeleo ya Jamii.
Mmoja wa Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wilaya ya Chamwino Bi. Sophia Swai ameishukuru Wizara na kuiomba iendelee kushirikiana nao katika kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Jamii kwa manufaa ya Jamii.
Sekta ya Maendeleo ya Jamii ni Sekta muhimu sana katika Ustawi wa jamii na katika kuletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

No comments