Header Ads

Responsive Ads Here

SERIKALI INATAMBUA UKATILI WANAOKUMBANA NAO WATOTO


interview

Na Mahmoud Ahmad Arusha
Serikali inatambua ukatili wanaokumbana nao watoto ndio maana imeandaa mkakati wa taifa wa kukabiliana changamoto 8 zitakazo shuhulikiwa ili kutatua na kupunguza masuala ya ukatili hapa nchini wanazokumbana  wazee,watoto na kinamama

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Dkta Hamis Kigwangala wakati wa ufunguzi wa mkutano wa huduma ya malezi na masaada wa kisaikolojia kwa watoto uliondaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Repssi unaondelea jijini hapa.
Dkta Kigwangala amesema kuwa kulikuwa na mikakati zaidi ya 8 na sasa wanakuja na mkakati mmoja unaoanza mwaka huu hadi mwaka 2022 lengo kuu ni kupambana na ukatili dhidi ya ustawi wa maendeleo ya motto na kutoa ushauri nasaha utakaosaidia taifa siku za usoni kimaendeleo.
Amesema kuwa mikakati mingi imelenga kuondoa suala zima la ukatili na mkutano huo utasaidia kuja na njia nzuri ya kuweza kusaidia taifa letu kuondokana na ukatili wa kijinsia ambao unashika kasi hapa nchi kwani takwimu zinaonyesha kati ya watoto saba mmoja amefanyiwa kuatili uwe wa kingono au kufanyishwa kazi.
“Mkakati huu mmoja utasaidia kurahisihsa kujenga mwamko wa uelewa kwani tatizo letu linafanana kwa bara la Afrika ni suala zima la uwelewa wa masuala ya ukatili hivyo ni jukumu letu sote kutoa elimu kwa wananchi wetu juu ya ukatili kwa watoto na elimu ya saikolojia”alisema Dkta Kigwangala.
Kwa Upande wake Katibu mkuu wa Afrika mashariki Balozi Leberat Mfumukeko amesema kuwa Jumuiya ina mpango mkakati kwa kuzitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuhakiksha wanazipa kipaumbele masuala ya watoto katika ustawi wa kijamii na maendeleo ya bara hili ambapo watoto asilimia 50% wanaishi katika mazingira hatarishi katika nchi za jumuiya hiyo.
Amesma kumekuwapo na mambo mbali mbali yanayochangia watoto kukuwa wakikosa ushauri nasaha na wengine wakikumbwa na ukatili kwa kukosa huduma za Afya lishe duni haki za ustawi wa watoto sisi tukiwa na mip[ango ya kimaendeleo kama hatukuwapa kipaumbe watoto hapo siku za usoni tutashuka kimaendeleo kwa kukosa nguvukazi imara.
Nae mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Dodoma Fatma Tawfiq amesma kuwa ukosefu wa elimu ya jinsia kwa watoto ikiwemo elimu ya Afya ya uzazi imechangia watoto kutoweza kuzifikia ndoto zao na kuwataka wazazi barani Afrika kuanza kuwapa nafasi watoto wao kuweza kujieleza hii itasaidia hata taifa kimaendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa taasisi ya REPSSI Bi Edwick Mapalala alisema kuwa mkutano huo unawakutanisha wataalamu wa masuala ya watoto kutoka ndani ya serikali za nchi 13 na wadau kutoka taasisi ziosizo za kiserikali mashirika ya umoja wa mataifa na yale yanaohusika na masuala ya watoto pande zote za ulimwengu lengo kuu ni kuelimishana na kufundishana katika kuhudumia na kukabiliana na masuala mtambuka yahusuyo watoto.

No comments