Header Ads

Responsive Ads Here

SCHALKE 04 WAUTAMANI USHINDI DHIDI YA BAYERN MUNICH LIGI YA BUNDESLIGA,MUBASHARA LIVE STARTIMES KESHO


arturo-vidal-nabil-bentaleb-bayern-munich-schalke-04022017_znts6x555dhz1t84zi9nmeefp
Kila mara Schalke wanapocheza na Bayern Munich kwenye Bundesliga, mashabiki wa Schalke huwa wanakumbuka jinsi timu yao ilivyoichapa Bayern 7-0 katika uwanja wao wa nyumbani, Allianz Arena.

Lakini hali hubadilika wakikumbuka mechi hiyo ilichezwa mwaka 1976, na tangu kipindi hicho ushindi au walau Sare vimekuwa adimu dhidi ya mabingwa mara 27 wa ligi ya Bundesliga.
Ni kweli Schalke walishinda tena 5-1 lakini hata hiyo ni miaka 15 iliyopita.                  Schalke wameshinda mara moja tu kaika mechi 18 zilizopita dhidi ya Bayern huku mabingwa Bayern wakishinda jumla ya michezo 13 na ni michezo mine tu iliyomalizika kwa sare.
Kitu kingine cha kuumiza zaidi kwa mashabiki wa Schalke ni kukumbuka mwaka 2001 walipokuwa Mabingwa kwa dakika 4 na sekunde 38!! Schalke walikuwa wameshinda mchezo wao wa mwisho huku Bayern akiwa anapoteza dhidi ya Hamburg. Schalke walijua tayari wameshanyakua Ubingwa kwa mara ya kwanza, lakini shangwe zao zilikatishwa baada ya kupata taarifa Bayern Munich wamesawazisha katika dakika ya tano ya Majeruhi na hatimaye kubeba Kombe la Bundesliga kwa mara nyingine tena.
Baada ya kupoteza mchezo ulipita dhidi ya Hoffenheim kwa 2-0, Bayern Munich wameshinda mchezo wao wa kwanza kwenye UEFA mwaka huu kwa kuwafunga Anderlecht 3-0 japokuwa kiwango chao hakikuvutia sana.
Lakini tatizo haliko tu ndani ya uwanja bali hata nje ya uwanja pia, Staa Robert Lewandowski alishukiwa na Maafisa wa klabu hiyo baada ya kufanya mahojiano huku akiponda usajili waliofanya bila, naye Franck Ribery ameshutumiwa kwa kutupa jezi yake baada ya kufanyiwa Sub katika mechi dhidi ya Anderlecht.
Muholanzi Arjen Robben alinukuliwa akisema kwamba wachezaji wamekubali kuwa wanatakiwa kufanya vizuri zaidi ili kufikia malengo yao. “Hatujacheza vizuri kama tunavyopenda na tunavyotakiwa kufanya.
“Kama tunataka kutetea ubingwa wetu, tunatakiwa kufikia kiwango tulichokuwa nacho msimu uliopita”, alisema.
 Mechi hii ndiyo yenye ukubwa kabisa kaika mechi a katikati ya wiki na itaonyeshwa MUBASHARA saa 3:30 Usiku kupitia chaneli ya World Football ndani ya StarTimes ambao ndio  pekee wana kibali cha Kuonyesha matangazo hayo.
Vilabu hivi viwili vina utamaduni wa aina yake nchini Ujerumani, na hivi sasa Schalke yuko juu ya Bayern kwenye msimamo wa ligi huenda wakaamini wanayo nafasi nzuri ya kuwapa kipigo.
StarTimes pia inacho kibali cha kuonyesha Mashindano yanayosimamiwa na FIFA ikiwemo World Cup ya Russia mwaka 2018.

No comments