Header Ads

Responsive Ads Here

RC MASENZA: MARUFUKU WENYEVITI WA MITAA NA VIJIJI KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA ARDHI


Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza na wadau mbalimbali wa wilaya ya mufindi wakati wa kutambulisha mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga uliokuwa na lengo la kuonyesha dira ya miaka ya hamsini (50) ya maendeleo ya mji wa Mafinga ambapo inasemeka ni moja kati ya miji inayokuwa kwa kasi .
 Hawa ni baadhi ya wadau waliojitokeza katika ukumbu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya mufindi kushuhudia utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa mafinga.
………………………………………………………….
Na Fredy Mgunda, Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametaka wenyeviti wa vijiji  au
wa mitaa kutojihusisha na uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro ambayo imekuwa
ikisababishwa na viongozi hao.
 
Akizungumza wakati wa
utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga, Masenza alisema
kuwa kumekuwa na migogoro ambayo inasababishwa na wenyeviti wa serkali za
vijiji au mtaa hivyo ni marufuku viongozi hao kujihusisha na swala hilo.
 
“Sipendi kusikia mwenyekiti
wa mtaa au mwenyekiti wa kijiji akihusisha kuwa shahidi wa uuzwaji wa ardhi kwa
kuwa hilo sio jukumu lao waichie mamlaka ya ardhi kufanya kazi kwa utaalamu
wao”alisema Masenza
 
Aidha Masenza alimtaka
wakurugenzi wote wa mkoa wa iringa kuwaambia ukweli viongozi juu ya sheria ya
uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro inayosababisha maumivu kwa upande unaonewa
na kudhurumiwa haki yao ya msingi na kusababisha kumrudisha nyuma kimaendeleo.
 
“Wakurugenzi waambieni
vijana wetu waache ujanja ujanja wa kupokea,kuchora,kuonyesha na kuelekeza
swala lolote linalohusu uuzwaji wa ardhi ili hii mipango kabambe ya halmashuri
ziende vizuri kama serikali inavyopanga”alisema Masenza
 
Masenza alisema kuwa acheni
kufanya kazi kwa ujanja ujanja maana serikali ya uwamu ya tano chini ya uongozi
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe maguli haitaki
wananchi na viongozi kuishi kwa mazoea.
 
Sixbet Kayombo ni mwenyekiti
wa serikali ya mtaa wa Balali katika halmashauri ya mji wa Mafinga alisema kuwa
tamko la mkuu wa mkoa lianukweli ndani yake kwa kuwa kuna wenyeviti wengi
wamekuwa wakisababisha migogoro isiyokuwa na maana kwa uroho wa kupokea pesa.
 
“Lakini ukiangalia kwa
undani utagundua kuwa haiwezekani wananchi kuuza ardhi bila kuwepo ushaidi wa
serikali ya mtaa hivyo tunamuomba mkuu wa mkoa kutafuta njia mbadala ili
mwananchi asiwe na ukakasi wowte wakati wa uuzaji wa ardhi yake” alisema
Kayombo
 
Naye mwenyekiti wa mtaa wa
Amani kata ya Upendo Merikioni Ndelwa
alisema kuwa tatizo hilo limekuwa kubwa hasa vijijini kwa kuwa viongozi
wengi bado hawana elimu ya mwisho wa madaraka yaho hivyo tunamuomba mkuu wa
mkao kutoka elimu wa wenyeviti ili kuepusha migogoro ya ardhi.

No comments