Header Ads

Responsive Ads Here

RC MASENZA AUPONGEZA MPANGO KABAMBE WA HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA

mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza wakati wa mkutano wa utambuzi wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa mafinga wilayani mufindi mkoani Iringa

prof Aldo Lupala akitambulisha na kuelezea jinsi gani walifanikiwa kuundaa mpango huu kwa tija na maendeleo ya halmashauri ya mji wa mafinga
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga Charles Makoga akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza sambamba na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri williamu wakati mkutano wa utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa mafinga

Na Fredy Mgunda,IringaHalmashauri ya mji wa mafinga wilayani mufindi mkoani Iringa yajipanga kuwa manispaa kwa kuanza kuupanga mji kuwa wa kisasa na wakibiashara kwa kutumia wataalamu kutoka chuo cha SUA na wataalamu kutoka halmashauri hivyo.

Akizungumza wakati wa kikao cha mpango kabambe wa mji wa mafinga mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa mji wa mafinga unatakiwa kukuwa kwa mpangilio unao stahili hivyo kuanza na mpango huu itakuwa njia mbadala ya kutatua changamoto mbalimbali za miundo mbinu ambazpo mikoa mingine kuna migogoro mingi.

“Niwashukuru wataalamu na viongozi wa halmashauri hii kwa kazi kubwa mliyoifanya ya kubuni na kuanzisha mpango kabambe ambao utakuwa mfano kwa halmashauri nyingine zinazokuwa kwa kasi  na  hazina mpango kama huu” alisema Masenza 

Masenza aliwataka viongozi na wadau wa maendeleo katika halmashauri hiyo kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya mpango huo kabambe ambao utasaidia kukuza mji kwa kasi na kuwa na mpangilio unaotakiwa hapa nchi.

“Sasa naona tuliopo hapa tunatosha kufikisha ujumbe huu kwa wananchi na wadau wengine ambao hawajahudhuria mkutano huu ili jamii kuwa na elimu na kuondoa migogoro na minong’ono iliyopo kwa wananchiwasiojua chochote kuhusu mpango huu” alisema Masenza

Aidha masenza aliwashukuru wataalamu kutoka chuo SUA kwa kufanikisha mpango kabambe huo kwa gharama nafuu tofauti wangepewa makampuni binafsi ambao mara nyingi gharama zao huwa juu sana tofauti na taasisi za kiserikali na kuitaka halmashauri ya mji wa mafinga kuendelea kuzitumia taasisi za kiserikali zenye uwezo na vigezo stahili kweli miradi mbalimbali ya mji wa mafinga.

Kwa upande wake mwenyekiti ya halmashauri ya mji wa mafinga Charles Makoga alisema kuwa mpango kabambe huu utadumu kwa takribani miaka hamsini ijayo hivyo wakazi wa halmashauri hiyo watanufaika kwa kuwa na mji ambao utakuwa umepangiliwa kwa kila kitu.

“Mkuu wa mkoa nikuahidi kuwa mpango huu utakuwa wa miaka mingi na tutafuata mambo mazuri yote kutoka kwa wataalamu ili kuufanya mji wa mafinga kuwa kivutio cha miji mingine na kuwafanya watu wenngine kuiga mfano kutoka kwetu” alisema Makoga

Makoga aliwapongeza wanafunzi, wataalamu wa chuo cha SUA pamoja na wataalamu kutoka halmashauri kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya  kuhakikisha mpango huo kukamilika kwa wakati pasipo kuwa na changamoto zozote zile.

Halmshauri ya mji wa mafinga tunategemea hivi karibuni kuwa manispaa kwa kuwa vigezo karibia vyote tunavyo hivyo tunaomba kuendelea kushirikiana na kushauriwa katika mikakati ya kuukuza mji huu unakabiliwa na ongezeko la watu kila siku alisema Makoga.

Naye prof. Aldo Lupala alisema kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na wataalamu wengi hivyo ni vyema wakatumiwa katika miradi mingi ya kimaendeleo ili kungeza ajira na kukuza ujuzi wao pindi wawapo kazini.

“Unajua ukiwa mtaalamu halafu huna kazi kwa kiasi fulani utaalamu au ujuzi wake utapungua toafuti kila wakati mtaalamu akiwa kazini huongeza ubunifu na kukuza utaalamu wake hivyo mgeni rasmi naomba tufikishie ujumbe huu serikali kuu” alisema Lupala

Prof Lupala aliupongeza uongozi wa halmauri ya mji wa mafinga kwa kufanya kazi na wataalamu kutoka chuo kikuu cha SUA kwa ushirikiano mkubwa ambao umefanikisha kupata mpango kabambe ambao utaisaidia halmashauri kwenye mipango ya kuukuza miji huo wa mafinga kuwa manispaa.

No comments