Header Ads

Responsive Ads Here

RAIS WA RT,MHE.MTAKA KUFANYA KIKAO NA WAANDAAJI (RACE ORGNISERS) WA MBIO NDEFU TANZANIA SEPT 16,2017


Anthony Mtaka
 
 
RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Mh. Anthony Mtaka, kwa kutambua mchango mkubwa wa wadau mbalimbali katika maendeleo ya mchezo wa riadha hapa nchini, ameandaa kusanyiko (kikao cha pamoja), na waandaaji mbalimbali wa mbio ndefu hapa nchini.

Waandaaji wa matukio mbalimbali ya mchezo wa raidha hapa nchini, kwa namna moja ama nyingine wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya mchezo wa riadha hapa nchini na jamii kwa ujumla, hivyo kwa kutambia hilo, RT imeona kuna umuhimu mkubwa Kamati yake ya Utendaji ikakutana na waandaaji hao katika uboreshaji.
Itakumbukwa kwamba, hivi sasa kumekuwa na uibukaji mkubwa wa watu mbalimbali kuandaa matukio hayo ya riadha bila kufuata taratibu na kanuni zilizopo kisheria na kikanuni hivyo kupoteza lengo tajwa la mchango wa kimaendeleo katika mchezo na jamii kwa ujumla.
Hivyo RT inaamini kupitia kusanyiko hilo litakalofanyika Septemba 16 mwaka huu kwenye ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi litaibuka na maazimio chanya ya kuweka taratibu na miongozo sahihi kwa pande zote, ikiwamo taratibu za uandaaji wa matukio ya riadha, viwango vya matukio hayo, pia mpishano wa tukio moja na jingine bila kuingiliana (Kalenda),.
Hivyo tunapenda kutoa wito kwa waandaaji wote, ambao tayari tunaamini wameishapata wito ‘official’ watajitokeza bila kukosa.
RT inapenda kuwashukuru Kampuni ya MultChoice Tanzania ‘DStv’ kufanikisha tukio hili kwa manufaa ya maendeleo ya mchezo wa Riadha Tanzania.
Itakumbukwa, DStv kwa muda sasa, wamekuwa washirika wazuri katika kuchangia maendeleo ya mchezo wa raidha Tanzania, ikiwamo kufadhili kambi za timu zetu za Taifa na hata kwa wanariadha mmoja mmoja, akiwamo Mshindi wa Medali ya Shaba katika mashindano ya Dunia, Alphonce Felix Simbu .
 
MBIO MBALI MBALI ZINAZOENDESHWA
HAPA NCHINI
 
                                JINA LA MBIO                                 INAKOENDESHWA
 
1.      KILIMANJARO INTERNATIONAL MARATHON –           KILIMANJARO
2.      KILFM HALF MARATHON                                –           KILIMANJARO
3.      HEART HALF MARATHON                               –           DAR ES SALAAM
4.      NGORONGORO  HALF MARATHON                –           MANYARA
5.      KARATU  10KM                                                –           MANYARA
6.      BABATI  HALF  MARATHON                            –           MANYARA
7.      TULIA HALF MARATHON                                 –           MBEYA
8.      SEREBUKA  HALF  MARATHON                       –           SONGEA
9.      TANGA HALF MARATHON                               –           TANGA
10.  MT. MERU MARATHON                                  –           ARUSHA
11.  DAR  ROTARY  INT. MARATHON                    –           DAR ES SALAAM
12.  BAGAMOYO  HALF  MARATHON                    –           PWANI
13.  10KM                                                               –           ARUSHA
14.  KIA  HALF  MARATHON                                   –           KILIMANJARO
15.  SERENGETI MARATHON                                 –           SIMIYU
16.  ROCK CITY  MARATHON                                 –           MWANZA
17.  IGOMBE  HALF  MARATHON                          –           TABORA
18.  MEI  DAY HALF MARATHON                           –           DAR  ES  SALAAM
19.  IKUNGI  HALF MARATHON                              –           SINGIDA
20.  NAMTUMBO HOSPITAL FUND RAISING          –           SONGEA
21.  ARUSHA TOURISM HALF MARATHON            –           ARUSHA
 
IMETOLEWA NA WILHEM GIDABUDAY
KATIBU MKUU RT
SEPTEMBA 12, 2017
 

No comments