Header Ads

Responsive Ads Here

Puma kutoa Zawadi Ya Milioni 2/- Kwa Mshindi


Na Mwandishi Wetu
-DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Puma Enegy Tanzania,  imehitimiza mashindano ya uchoraji picha za usalama barabarani kwa shule za Msingi kwa mwaka 2017 kwa kutoa kutoa zawadi ya Sh milioni 2 kwa mshindi wa kwanza.

Akizungumza jijini Dar e Salaam jana Mkurugenzi Mkuu wa Puma Enegy Tanzania Ltd, Philippe Corsaletti, alisema kuwa mashindano ya mwaka huu yalihusisha jumla ya shule 14 za mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro ambapo washindi hao walipatikana jana.
Katika mashindano hayyo mshindi wa kwanza aliyeibuka ni Nasri Mwema wa Shule Msingi Amani katika shindfano hilo lililoshirikisha shule 14.
 “Mshindi huyu wa kwanza atapata kikombe na cheti ambapo shule anayotoka itapata fedha Shilingi milioni 2 ambazo zitatumika kwa ajili ya kununulia vitabu. Shindano hili la usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa njia ya uchoraji linalenga kusaidia kuelimisha wanafunzi wa shule za msingi katika masuala ya usalama barabarani.
“Mpango wetu wa usalama barabarani kwa shule hapa nchini Tanzania ulianza tangu mwaka 2013 na mpaka sasa shule za msingi zipatazo 47 zimeshashiriki zikiwa na jumla na wanafuzni 60,000 kutoka mikoa mbalimbali,” alisema Corsaletti
Mkurugenzi huyo wa Puma Enegy, alisema kuwa shindano hilo la usalama barabarani kwa njia ya uchoraji linalenga kumpatia kila mwanafunzi nafasi ya kushirikisha mawazo yake juu ya namna bora ya kuboresha usalama barabarani ambapo kati yao huchaguliwa washindi na kuzawadiwa.
“Lengo letu la muda mrefu ni kufikia shule zote hapa nchini ziweze kushiriki katika mpango huu. Kampuni ya Puma Enegy imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani pamoja na SUMATRA katika masuala mbalimbali yahusuyo usalama barabarani.
“Tunaamini kwamba ajali za barabarani zinaweza kupungua kwa kiasi kikubwa ikiwa pande zote zinazohusika ambazo ni pamoja na madereva, wenye magari na wasimamizi wakitekeleza wajibu wao ipasavyo. Jukumu letu pamoja linabaki kuwa wajibu shirikishi katika kutengeneza mazingira salama kwa ajili ya watoto wetu na vizazi vijavyo,” alisema alisema
Naye Msajili wa Hazina, Dk. Osward Mashindano, alisema kilichofanywa na Kampuni ya Puma ni jambo jema ambalo litasaidia katika kuiandaa jamii kuepuka ajali za barabarani.

No comments