Header Ads

Responsive Ads Here

Prof. Maghembe Kufungua Maonesho ya Utalii Iringa leo


iringa1
Mhandisi Kerdick Chawe (kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (mwenye ushungi) kwenye banda la maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wanaoshiriki kwenye maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.

iringa2
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesela  (kulia) akisalimiana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa kilichopo Kata ya Nduli, katika banda la maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
iringa4
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Bahati Mollel akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesera katika banda lao la maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
iringa6
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Katioliki cha Iringa (RUCU), wakipata maelezo mbalimbali ya viwanja vya ndege kutoka kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa kilichopo Kata ya Nduli, Bi. Hana Kibopile katika maonesho ya Utalii  ya Karibu Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
iringa8
Meneja wa SUMATRA mkoa wa Iringa, Mhandisi Patel Ngereza(kushoto),akimsikiliza maelezo mbalimbali kutoka kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Iringa kilichopo kata ya Nduli,Bi. Hana Kibopile katika maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwenye Viwanja vya Kichangani mkoani  Iringa.
iringa11
Mhandisi Kedrick Chawe (wa pili kushoto), akimpa maelezo mbalimbali Bw. Nathan Hesketh wa Iringa alipotembelea banda la maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
………………..
Na Mwandishi Wetu,Iringa
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe leo atafungua rasmi maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim, yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
Maonesho hayo yenye kaulimbiu ya Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda yanashirika taasisi za serikali, mashirika ya umma na kimataifa zaidi ya 400, ambapo yatamalizika Oktoba 2, 2017, ambapo yanalengo la kuweka uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa utalii na thamani thamani ikiwa ni pamoja na kuutangaza utalii kwa kuihamasisha jamii kutumia fursa za utalii zilizopo katika kuinua uchumi wa wakazi wa Ukanda wa Kusini mwa Tanzania na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa Wizara mbalimbali zipo na taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Idara ya Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale na Misitu na Nyuki, Chuo cha Taifa cha Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mamlaka ya Usimamizi ya Wanyamapori (TAWA) Mfuko wa Misitu Tanzania  (TaFF).
Taasisi nyingine ni Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS)  Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii.Wadau wa Sekta ya Utalii kutoka mikoa  ya Nyanda za Juu Kusini watashiriki kuonesha bidhaa na huduma zao muhimu na mikoa inayoshiriki ni pamoja na wenyeji Iringa, Mbeya, Ruvuma, Songwe na Njombe.
Fursa zilizopo nyanda za Juu Kusini ni pamoja na Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa,  Ismila,Kalenga na Boma la Mkuu wa Wilaya, Hifadhi za Mahale, Katavi, Ruaha, Kitulo na Selous.

No comments