Header Ads

Responsive Ads Here

Prof. Maghembe Afungua Maonesho ya Utalii

msigwa1
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (kushoto),aliyefungua rasmi maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini,  akikaribishwa na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa kilichopo Kata ya Nduli  kwenye banda la maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani..
msigwa2
Mhandisi Kedrick Chawe (kulia) akisalimiana na mgeni rasmi wa maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini, Waziri wa Maliasili na utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (mwenye ushungi mweupe) na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesela.
msigwa3
Mbunge wa Iringa, Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) akisalimiwa na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa kilichopo Kata ya Nduli, Bi. Hana Kibopile alipotembelea banda la maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini  la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
msigwa4
Afisa Usalama wa Kiwanja cha ndege ckha Iringa kilichopo kata ya Nduli, Bw. Miyaga Watanda (kulia) akitoa maelezo mbalimbali kwa wanafunzi wa shule ya Wasichana ya Iringa walipotembelea banda la maoneksho ya Utalii ya Karibu Kusini la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).  

No comments