Header Ads

Responsive Ads Here

NAIBU WAZIRI WA ARDHI AZIONYA HALMASHAURI ZINAZOTELEKEZA NYUMBA ZA NHC


ardhi14
Na. Hassan Mabuye
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabulla amezionya halmashauri nchini ambazo zinaomba kujengewa Nyumba na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na baada ya Shirika kuwajengea wanazitelekeza.

Mhe Mabulla ameyasema hayo wakati alipofanya ziara Mkoani Shinyanga na kugundua kati ya nyumba 50 zilizojengwa na NHC kwa ajili ya Halmashauri Kahama ni  nyumba 1 tu ambayo imenunuliwa, licha ya kuwa halmashauri hiyo ndio iliomba kuje gewa nyumba hizo.
Huwezi kuomba kitu halafu kwenye kukichukua iwe ni ugomvi, kwa hiyo sasaivi naielekeza Shilika la Nyumba la Taifa hakuna kujenga nyumba mpya mahala popote kama huna makubaliano ya wali na Halmashauri husika. Amesema Mhe. Mabulla
Katika hatua Nyingine Naibu Waziri huyo ameendelea kuwabana maafisa wa ardhi ambao hawasimamii makusanyo ya kodi ya pango la ardhi ipasavyo na kuto kuwashughulikia.
Mabulla aliwataka maafisa adhi wa halmashauri ya Shinyanga kumpatia majina ya wadaiwa sugu 100 wa awali ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi kwa miaka mitano iliyopita ili wafikishwe mahakamani au mali zao kupigwa mnada.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bibi Zainab Tellack ametumia nafasi hii kumuomba Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabulla kumsaidia kutatua baadhi ya migogoro inayoukabili mkoa wa Shinyanga kabla ya kuondoka.
Katika kusimamia hilo Mhe. Mabulla alitembelea masijala ya ardhi ambayo hutumika kuhifadhia kumbukumbu na nyaraka za zinazohusu hatimiliki na kumuagiza Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Magharibi kuwaelekeza jinsi ya kutunza kumbukumbu maafisa wa ardhi wa halmashauri ya Shinyanga ili kuepuka migogoro.

No comments