Header Ads

Responsive Ads Here

NAIBU WAZIRI JAFO AZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI KUELEKEA SIKU YA KILELE OKTOBA MOSI 2017 MJINI DODOMA


Pix 1
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo( wa pili kushoto) akiwasili katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma kuzindua Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani kwa kuzindua maonesho ya shughuli za wazee za ujasiriamali, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto Bw. Julius Mbilinyi .

Pix 2
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akiangalia moja ya bidhaa zilizopo katika  mabanda ya maonesho ya shughuli za wazee za ujasiriamali katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma kabla ya kuzindua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.
Pix 3
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee Tanzania Mzee Sebastian Bulegi akitoa salamu za wazee kwa Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (hayupo Pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Pix 4
Kaimu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto Bw. Julius Mbilinyi akitoa neno kwa niaba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na Watoto kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Pix 5
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Pix 6
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wazee katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma wakati akizindua Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.
Pix 7
Baadhi ya wazee kutoka mikoa mbalimbali Tanzania wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma kwenye uzinduzi wa  Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.
Pix 8
Kikundi cha Ngoma cha Lusombi kutoka Ruvuma  kikiburudisha kwenye uzunduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Pix 9
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yanayofanyika kwa mwaka 2017 Mjini Dodoma kwa kauli mbiu isemayo :“Kuelekea Uchumi wa Viwanda:Tuthamini Mchango,Uzoefu na Ushiriki wa Wazee kwa Maendeleo ya Taifa”
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

No comments