Header Ads

Responsive Ads Here

MUFTI WA TANZANIA AMTEMBELEA RC MAKONDA


index
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametembelewa Ofisini kwake na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zuber na kufanya Mazungumzo.

Katika Mazungumzo hayo Mufti amemtia Moyo Makonda na kumsihi asikate tamaa sababu kazi anayoifanya ni Njema na inagusa watu wa makundi  yote hususani Wanyonge.
Aidha Mufti amemuunga mkono RC Makonda kwa kumletea mdau atakaejenga Ofisi za Walimu kwenye Shule tatu.
“Nimeona nisikae kimya ndio maana nimeona niunge mkono Kampeni yako ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu kwa kutafuta mdau ambae atajenga Ofisi kwenye Shule Tatu ili Walimu wafanye kazi kwenye mazingira mazuri” Alisema Mufti.
Makonda amemshukuru Mufti kwa kumtembelea na kusema kuwa ataendelea na jitiada zake za kufanya kazi kwa bidii ilikutatua changamoto za Wakazi wa Dar es salaam.
Aidha Makonda amewaomba Viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa kujitoa kwa pamoja ili kuijenga Dar es Salaam.

No comments