Header Ads

Responsive Ads Here

MSUVA AZIDI KUITEKA MOROCCO,APIGA MBILI STARS IKIIDUNGUA 2-0 BOTSWANA MECHI YA FIFA


IMG_8241
Mchezaji wa zamani wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom timu ya Yanga na winga wa Kimataifa na klabu ya  Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva amefunga magoli mawili kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA.

Msuva alikuwa ni miongoni mwa wachezaji watatu waliocheza kwa mara ya kwanza Stars tangu walipopata nafasi ya kucheza nje ya nchi. Hamisi Abdallah anayecheza Sony Sugar ya nchini Kenya  na Abdi Banda akitokea timu ya Baroka FC ya Afrika Kusini ni wachezaji wengine ambao wamecheza kwa mara ya kwanza tangu waliposajiliwa nje ya nchi.
Goli la kwanza la Stars limefungwa dakika ya tano  kipindi cha kwanza ampapo Msuva alimalizia kazi pasi safi ya Mzamiru Yassin huku bao la pili likifungwa dakika ya 61 kipindi cha pili ambapo Kichuya alifanya kazi ya ziada iliyomaliziwa kwa ustadi na Msuva.
Stars ilipata ushindi wa magoli 2-0 March 25, 2017 ushindi ambao imeupata tena leo Septmber 2, 2017 yote ikiwa ni michezo ya kirafiki ndani ya miezi saba.

No comments