Header Ads

Responsive Ads Here

Miss Vyuo Vikuu sasa kufanyika Oktoba mwishoni


IMG-20170923-WA0062-1
 Warembo wa wanaowania taji la mrembo wa vyuo vikuu vya Tanzania “Miss Higher Learning Institution 2017” wakiwa katika picha ya pamoja.  Shindano hilo lililopangwa kufanyika Septemba 29, limehairishwa mpaka mwishoni mwa mwezi ujao.

IMG-20170923-WA0063-1IMG-20170923-WA0064-1
 Warembo wa wanaowania taji la mrembo wa vyuo vikuu vya Tanzania “Miss Higher Learning Institution 2017” wakiwa katika picha ya pamoja.  Shindano hilo lililopangwa kufanyika Septemba 29, limehairishwa mpaka mwishoni mwa mwezi ujao.
……………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam.  Mashindano ya kumsaka mrembo wa vyuo vikuu vya Tanzania “Miss Higher Learning Institution 2017” yaliyopangwa kufanyika kesho Ijumaa ( Septemba  29)  kwenye ukumbi wa King Solomoni, Namanga jijini yamehairishwa.
Kuhairishwa kwa mashindano hayo kumetokana na sababu za kalenda na waandaaji kufikia makubaliano ya kusogeza mbele mpaka mwishoni mwa mwezi ujao.
Mashindano hayo yameandaliwa na kampuni ya Glamour Bridal Tanzania baada ya kupewa idhini ya waandaaji wa Miss Tanzania, Lino International Agency kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).
Mkurugenzi wa Glamour Bridal Tanzania Muba Saedo alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa kwa lengo la kuboresha zaidi na hatua hiyo itawawezesha kufanya mashindano yenye upinzani wa hali ya juu kutokana na idadi ya vyuo mbalimbali vilivyothibitisha.
“Tumelazimika kusogeza mbele mashindano kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wetu, warembo wataendelea na kambi chini ya mkufunzi wao Clara Michael na ba matron, Blessing Ngowi,” alisema Saedo.
Mbali ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), mashindano hayo yatashirikisha vyuo vya Taasisi ya Uhasaibu Dar es Salaam (TIA), IFM, CBE, UDOM, Tumaini – Makumira na Taasisi ya Uhasibu wa Arusha (IAA) na Chuo Kikuu Cha Ardhi.
Saedo alivitaja vyuo vingine kuwa ni Mzumbe, Chuo Kikuu cha Iringa, Tanzania Aviation University College na Magogoni.

No comments