MIAKA MITANO JELA KWA KUSAFIRISHA BINADAMU

Na Mwandishi Maalum,
Jackline Milinga (23) na wenzake wawili wamehukumiwa kwenda jela miaka mitano kila mmoja au kulipa faini ya Sh. Milioni 10 baada ya kukutwa na hatia ya usafirishaji wa binadamu.
Hukumu hiyo ilitolewa jana ( jumatano ) na Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Kisutu baada ya kujiridhisha na ushahidi usiotia shaka uliowasilishwa na upande wa mashtaka.
Wengine waliohukumiwa pamoja na Jackline Milinga ni Mary Amukowa ( 29) raia wa Kenya na Simon Mgaya.
Wasichana hao kumi waliokuwa na umri kati ya miaka 17 na 21 walikamatwa tarehe September 4, 2015 katika eneo la Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya wakiwa katika harakati za kuingizwa nchini Kenya. Wote walikuwa ni wakazi wa Dar es Salaam.
Maafisa wa Uhamiaji waliwatilia shaka wasichana hao baada ya kuwaona wakiwa wanarandaranda katika eneo hilo, na walipowahoji walisema, walikuwa wakiwasubiri ‘mabosi ‘ wao ambao walikuwa wakiwapeleka nchini Kenya kwenda kufanya kazi Saloni.
Mabosi hao Jackline na Mary walikuwa wameshavuka mpaka na kuingia nchini Kenya kuendelea na taratibu nyingine za kuwavusha wasichana hao.
Maafisa wa uhamiaji walipowapekua zaidi wasichana hao walikuta kwenye mabegi yao nguo za ajabu ajabu, vipodozi na viatu virefu, vitu ambavyo havikuashiria kwamba wasichana hao walikuwa wakienda kufanya shughuli halali.
Baada ya kujionea mavazi hayo, Maofisa hao waliwataka wasichana hao kuwapigia simu kuwapigia simu mabosi wao na waliporudi upande wa Tanzania walikamatwa.
Baada ya Jackline Milinga na Mary Amukowa kufanyiwa mahojiano walimtaja Simon Mgaya ambaye walikuwa wakishirikiana naye katika kuwatafuta wasichana waliokuwa na vigezo walivyovihitaji na pia alisaidia katika upatikanaji wa hati za kusafiria za muda kwa wasichana wawili kati ya kumi waliokuwa wakisafirishwa.
Mawakili wa Serikali walioendesha kesi hiyo Jacline Nyatori na Estazia Odhiambo walileta mashahidi 12 wakiwamo wasichana wanne kati ya wale kumi,Maafisa Uhamiaji, Polisi , Polisi wa Interpol na mtaalamu wa uhalifu wa mitandaoni, ambaye alisaidia kupatika kwa vielelezo kadhaa zikiwamo picha za wasichana hao.
Mawakili wa Serikali Nyatori na Odhiambo waliiomba Mahakama kutoa adhabu ya kifungo kisichozidi miaka 10 na kisichopungua miaka miwili na faini ya kuanzia milioni tano na isiyozidi milioni 100.
Mawakili hao katika maelezo yao walisema washtakiwa hao walistahili adhabu kali kutoka na kwamba walitenda kosa la udhalilishaji mkubwa kwa wasichana hao . Aidha walitaka adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine kutokana na ukweli kwamba kumekuwako na matukio mengi ya usafirishaji wa binadamu na.
Imetolewa
Ofisi ya Mwasharia Mkuu wa Serikali
Dar es Salaam
Post a Comment