Header Ads

Responsive Ads Here

MHASHAMU PAULO LUZOKA AOMBA JAMII IUNGANE KUWALINDA ALBINO.


shikuba
Na Tiganya Vincent-RS-Tabora
Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Tabora limeitaka jamii pamoja katika kuungana katika kuwalinda ,kuwaheshimu na kusihi nao watu wenye ulemavu wa ngozi ili nao waweze kutembea kifua mbele katika nchi hii kama walivyo watu wengine.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki mkoani Tabora Mhashamu Paulo Luzoka wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku mbili juu ya kuwahudumia watoto wenye ulemavu wa ngozi.
Alisema kuwa ni wajibu wa jamii nzima bila kujali tofauti zake za kiimani kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa haki ya kuishi watu wenye ulemavu wa ngozi inalindwa na kuwafanya waishi kwa amani na furaha.
Mhashamu Luzoka alisisitiza kuwa ni vema jamii ikaweka nguvu katika kuelimisha jamii kuachana na vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye ulemavu kwa imani za kishirikina ambavyo vinawafanya watu hao wasiishi kama watoto yatima.
Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuwafanya waishi bila hofu na hivyo kuwa huru katika kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yoyote ya nchi hii.
“Tusingependa kuona kuwa dawa ya watu hao ikendelea kumwagika kwa sababu ya ulemavu wao…jifikie wewe ungekuwa katika hali hiyo nawe ukatendewa kama wanavyofanyiwa watu hao ungejisikiaje ? kama wewe unapenda kutendewa jambo jema basi mtende na wewe albino jambo jema” alisema Askofu huyo wa Jimbo Kuu la Tabora.
Alisisitiza kuwa kama jamii itaungana na kuishi kwa amani basi hakutakuwepo na mauaji ya watu wenye ulemavu na wazee kwa sababu ya umri wao kuwa mkubwa na macho kubadilika.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alilishukuru Kanisa kwa mpango wa kukabiliana na unyanyapa kwa watoto wenye ulemavu katika jamii wakiwemo albino.
Alisema kuwa Serikali ya Mkoa wa Tabora itasimama imara kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuwakata watu wote wenye imani za kishirikina ambayo wamekuwa wakimwaga damu za watu wenye ulemavu wa ngozi kwa mawazo ya kijinga kuwa watapata utajiri.

No comments