Header Ads

Responsive Ads Here

MFUKO WA BODABODA ARUSHA WAFIKISHA MILIONI 200


index
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh.Mrisho Gambo anasema “Sikuwa na Godfather kwenye siasa zaidi ya Mungu pekee, Mama yangu alikuwa anachoma Maandazi na Sambusa na Baba yangu alikuwa Dalali.Ila kwenye maisha kuna “Destination” ambayo mtu anatakiwa kuchagua, nilihangaika kusoma kwa bidii. Na kumsaidia Mama kuuza Sambusa wakati wa mchana baada ya masomo.

Huu ni Upande mfupi wa historia yangu kwa wale wasioijua. Mara ya kwanza wakati nafika Arusha nilihitaji kufanya uongozi unaoacha alama nikawafikiria Bodaboda, Hawa ni kundi kubwa la vijana waliojiajiri kila nilipofika walinikatisha tamaa lakini sikurudi nyuma nilifanikiwa kuwapata wahisani wakanipa Pikipiki 200. Sikupenda  zile pikipiki tuzitoe bure niliwakusanya vijana kwa makundi tukawakopesha leo hii mfuko umefikisha milioni 200, Nataka kusema jambo moja tu vijana tufanye kazi na tuache kupigana majungu”

No comments