Header Ads

Responsive Ads Here

MBUNGE MSIGWA MATATANI TENA


Mbunge Msigwa akishuka  katika gari la  polisi (picha na maktaba ya matukiodaima)
Baraka  Kimata  kushoto akiwana  mbunge Msigwa enzi  hiyo akiwa Chadema
………………………………………………………………………………………………………………..
Na  MatukiodaimaBlog
ZIKIWA zimepita  siku  chache  toka  mbunge wa  jimbo la  Iringa  mjini  kupitia Chadema Mchungaji Peter Msigwa kukamatwa na  polisi  kwa  tuhuma za kutoa  lugha za kichochezi  kati ya   wananchi na dola mbunge huyo  leo  amekamatwa na  polisi tena kwa tuhuma za kumpiga aliyekuwa diwani wa Chadema kata ya  Kitwiru Baraka  Kimata .
Akizungumza na matukiodaima kwa njia ya  simu diwani  Kimata  alisema  kuwa tukio hilo limetokea eneo la viwanja  vya ofisi ya manispaa ya  Iringa wakati  akiwa katika wajibu  wake katika  ofisi  za Halmashauri .
”  Nilikuwa katika ofisi za manispaa kwa shughuli  zangu kama mkazi wa Manispaa nilipo toka nje  nilikutaka na mbunge Msigwa  nilisogea  kumsalimia ila  baada ya  kumsogelea alikataa salamu  yangu  na  kunitaka  niondoke  kuwa eti  hawezio   kupokea  mkono  wangu  kuwa nilimuita  yeye  dikiteta”
Kuwa baada ya  kukataa salama mimi niliondoka na  kuelekea katika gari  langu  na  baada ya  kuingia  ndani ya gari gafla  mbunge  alikuja na kuzuia mlango  nisifunge  na kuanza kunipiga akishirikiana na dereva  wake .
Alisema  kutona na  vurugu  alizovifanya na kumpiga ilipelekea  watumishi  wa manispaa ya  Iringa  kutoka na  kumsaidia  .
Baraka  amesema kuwa amefungua  kesi  kituo cha  polisi  kwa RB  namba   IR /RB /6498?2017  katika  kituo cha  polisi Iringa  mjini na  kuwa mbunge  huyo alikamatwa na  kupata  dhamana .
Jitihada za  kumpata  mbunge Msigwa kwa njia ya simu  hazijazaa matunda huku  jeshi la  polisi  limedhibitisha  kukamatwa kwake .
Diwani  Kimata  ni mmoja kati ya  madiwani  watatu  wa chadema  Iringa mjini  waliojiengua katika chama hicho  kwa madai ya mbunge  kuendesha  chama  hicho kidikteta  huku  diwani  wa nne  alifukuzwa chama kwa kosa la kulalamika  kupigwa katika  kikao  cha kumpata naibu  meya

No comments