Header Ads

Responsive Ads Here

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI MJINI DODOMA LEO SEPTEMBA 15,2017


1
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia Bunge leo mijini Dodoma muda mfupi kabla ya kuairisha Bunge hilo hadi mwezi Novemba 2017.

2
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjela Kairuki akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kunusuru Kaya masikini hapa nchini.
3
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akitoa ufafanuzi Bungeni kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha huduma za Afya katika vituo na Hosipitali zinazomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
4
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Tate Ole Nasha akieleza mikakati ya Serikali kukuza Sekta ya Kilimo hapa nchini kwa kuhakikisha kuwa wakulima wanapata pembejeo za Kilimo na mbolea kwa wakati
5
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge ajibu maswali ya wabunge leo Bungeni mjini Dodoma kuhusu hali ya upatikanaji wa maji hapa nchini na mikakati ya Serikali kuboresha kilimo cha umwagiliaji.
6
Mbunge wa Sumve Mhe. Richard Ndasa akizungumza Bungeni mjini Dodoma mapema leo.
7
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo akisisitiza jambo Bungeni mjini Dodoma mapema leo.
Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma

No comments