Header Ads

Responsive Ads Here

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI MJINI DODOMA LEO SEPTEMBA 11,2017


1
Waziri wa Habari  Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasilisha azimio la Bunge kuridhia mkataba  baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Uganda kuhusu mradi wa ujenzi wa Bomba la  Kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) leo Bungeni mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamamba Kabudi.

2
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo ya wabunge  mara baada ya kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.
3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akitoa maelezo kuhusu matumizi ya silaha   za jadi hapa nchini na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuzuia uzagaaji wa silaha hizo.
4
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Gerson Lwenge akitoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi katika Wilaya ya Ngara wanapata huduma za maji.
5
Naibu   Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia  injinia  Stella Manyanya akitoa  ufafanuzi kuhusu  jinsi  Serikali ilivyofanikiwa  katika   mpango wa elimu bure  hapa nchini.
6
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Tate Ole Nasha akizungumzia mkakati wa Serikali kuhakikisha kuwa Maafisa ugani katika maeneo yote hapa nchini  wanatekeleza majukumu yao ipasavyo katika kuwahudumia wananchi.
(Picha na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma)

No comments