Header Ads

Responsive Ads Here

MATOKEO VPL:VIWANJA SITA SARE ZATAWALA ‘NANGWANDA SIJAONA KICHEKO’


Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara wamebanwa na kulazimishwa suluhu kwenye Uwanja wa Uhuru na kikosi cha Mtibwa Sugar kutoka Turiani, Morogoro.

Hii ni mechi ya tatu Yanga wanatoka sare katika ligi ikiwa ni mechi ya tano tangu kuanza kwa ligi msimu huu. Wanajangwani walitoka sare kwa mara ya kwanza dhidi ya Lipuli kwenye mechi ya ufunguzi walipolazimisha sare ya kufungana 1-1.
Mara ya pili Yanga kutoka sare kwenye mchezo wa ligi ilikuwa mechi dhidi ya Majimaji FC ugenini kwenye uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma walipolazimisha matokeo ya kufungana 1-1.
Yanga wameshinda mechi mbili kati ya tano walizocheza, walishinda 1-0 ugenini dhidi ya Njombe Mji halafu wakapata ushindi wao wa pili dhidi ya Ndanda FC kwenye uwanja wa Uhuru.
Kwa Matokeo hayo Yanga wamefikisha pointi 9 huku Mtibwa Sugar wakiendelea kukaa kileleni wakiwa na pointi 11 na wakiwa hawajapoteza hata mechi Moja
Matokeo mengine kama ifuatavyo;
Mwadui FC 2-2 Mbeya City
Mbao FC 1-1 Tanzania Prisons
Singida 1-1 Azam FC
Majimaji 0–0 Kagera
Ruvu Shooting 1-1 Njombe Mji
Ndanda 2-1 Lipuli FC
Ligi hyo inatarajia kuendelea leo katika Uwanja wa Kambarage CCM mjini Shinyanga Chama la Wana ‘Stand United’ watawakaribisha wekundu wa Msimbazi Simba na kama Simba watapata ushindi moja kwa moja wataongoza Ligi.

No comments