Header Ads

Responsive Ads Here

MAKONDA AZINDUA MAJENGO YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO KATIKA ENEO LA MWANANYAMALA


PAU1
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akizindua  majengo yatakayotumika kwa ajili ya uanzishaji wa VIWANDA VIDOGO VIDOGO katika eneo la Mwananyamala manisapaa ya KINONDONI


PAU2PAU3
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali mkoa wa Dar es salaam.
PAU5
Katika kuunga mkono DIRA ya Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ya Tanzania ya VIWANDA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda AMEZIAGIZA manisapaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam kubadilisha Mfumo wa UTOAJI WA asilimia 10% kwa kina mama na vijana ili fedha hizo ziweze kuleta TIJA katika kutekeleza  DIRA ya taifa ya kuwa na Tanzania ya viwanda.
Mhe Makonda amesema mfumo wa sasa hauna UTAMBUZI wa kutosha kwa vijana na kimama kutokana na Makundi hayo kutawanyika kibiashara jambo linalosababisha changamoto ya ufuatiliaji wa mikopo hiyo, na badala yake Kuzitaka Manisapaa kutenga maeneo maalum ya uanzishaji wa VIWANDA VIDOGO VIDOGO kwa ajili ya makundi hayo, hatua itakayowaweka pamoja na hivyo kutoa fursa kwa serikali ya Mkoa kuwahudumia vizuri.
Mhe Makonda amesema katika kutekeleza Mpango huo Leo ameamua kuzindua majengo yatakayotumika kwa ajili ya uanzishaji wa VIWANDA VIDOGO VIDOGO katika eneo la Mwananyamala manisapaa ya KINONDONI ili kuzihimiza manisapaa nyingine kuiga mfumo huo.
Katika hatua nyingine, Mhe Paul Makonda AMEWATAKA wafanyabiasha NDOGO NDOGO (Machinga) kuanza kuuza BIDHAA zinazozalishwa nchini na viwanda vya wawekezaji walio Tanzania, pamoja na BIDHAA zinazozalishwa na wajasiriamali wadogo wadogo ili kuongeza wigo wa kukua kwa uzalishaji wa bidhaa zinazozalishwa Tanzania, amewataka WAMACHINGA nao kuonyesha UZALENDO kwa vitendo kama anavyofanya Rais Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli ambae siku zote ameonyesha MOYO na NIA ya kuwasaidia WAMACHINGA nchini.

No comments