Header Ads

Responsive Ads Here

MADIWANI 6 WASHIKILIWA NA POLISI GEITA KWA MAANDAMANO YA JANA MKOANI GEITA


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo akielezea juu ya hatua ambayo amechukua kwa kuwakamata madiwani sita pamoja na katibu wa UVCCM  Kutokana na kufanya maandamano ambayo yalikuwa ni kinyume na sheria za Nchi mbele ya waandishi wa habari.


Baadhi ya askari pamoja na wafanyakazi wa mgodi huo wakiwa kwenye Bomba ambalo linadaiwa kupasuliwa na Madiwani wa Halmashauri kwa maelezo ya wananchi ambao waliwaona wakifanya uharibifu huo.

Sehemu ya Bomba iliyoharibiwa ikitilili9sha maji kwa kasi kubwa zaidi kutokana na tukio ambalo limetokea siku ya jana kwa madiwani kuandamana wakishinikiza mgodi kuwalipa kiasi cha Dola Milioni 12.65 ambazo ni deni la mwaka 2004 hadi 2013. .

Meneja Mhandamizi wa Maswala ya Jamii Mgodi wa GGM ,Manase Ndoloma akiwa sehemu ya eneo ambalo lilifanyiwa uharibifu wa kupasuliwa kwa bomba ambalo ndio linapeleka maji kwenye chanzo cha maji mgodini hapo.

Shughuli za ukarabati wa Bomba hilo zikiendelea.

Mafundi wakiendelea na shughuli za ukarabati wa Bomba hilo.    

Madiwani 6 wanashikiliwa na Polisi mkoani Geita baada ya kufanya maandamano kinyume cha sheria na kusababisha uharibifu wa Bomba la Maji la kutoka Nungwe kwenda kwenye
Mgodi wa Dhahau wa GGM.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita Bw Mponjoli Mwabulambo amesema walichofanya madiwani hao jana hakikubaliki kisheria na kwamba hawakufuata utaratibu wa kufanya maandaman
yao na kwamba wanaendelea na msako wa kuwabahini wale wote ambao wamefanya
kitendo cha kuandamana na kusababisha baadhi ya kazi kusimama siku ya jana.
Amesema
miongoni mwa wanaoshikiliwa  ni pamoja na
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM
wilaya ya Geita kwa tuhuma za kushiriki maandamano na kufanya uharibifu
huo.
“Kwa mtu wa
kawaida sidhani kama alipendezwa na kitendo hicho tuache habari ya kuremba na
kupepesa macho lile tukio sidhani kama ni kitendo kizuri, ni kosa ambalo
walilitenda na kwamba tunawashikilia madiwani sita akiwemo katibu wa umoja wa
vijana wa chama cha mapinduzi wilaya ya Geita na hicho hakikuwa kizuri lakini
pia kukimbia kwao niseme sio suluhisho tutawakamata”Alisema Mponjoli.
Meneja
Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii kwenye mgodi wa GGM Bw Manase Ndoloma amesema
taarifa za kupasuliwa kwa bomba hilo linalotoa maji safi  kutoka ziwa Victoria kupitia kwenye kijiji
cha Nungwe hadi  kituo cha usambazaji
maji kwenye Bwawa la Nyakanga walizipata kwa wananchi na ameahidi kuendelea
kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao na kwamba
mgodi haujaathirika kwa kutobolewa kwa bomba hilo.
“Tungependa
kufanya shughuli zetu za kutekeleza miradi ya kuisaidia jamii ya Geita kwa hali
ya usalama lakini pia kwa usalama wa wafanyakazi wetu mgodi wa dhahabu wa Geita
utaendelea kushirikiana kwa ukaribu na serikali ya jamhuri ya muungano wa
Tanzania pamoja na jamii inayozunguka eneo la mgodi ili kuharakisha urejeshaji
wa maji pamoja na amani kwa ujumla ndani ya mji wa Geita”Alisema Manase.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Nungwe Bw  Revocatus Masatu
amesema aliwaona watu kutoka halmashauri na magari ya serikali na hakuwa na
taarifa yoyote kuhusu kupasuliwa kwa bomba hilo kwani alijua ni taratibu kwa
halmashauri kutembelea vijiji vyake.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE .

No comments