Header Ads

Responsive Ads Here

LEILA HAMOUD -WANAWAKE WAJITAMBUE KUPAMBANA NA HALI YA KIUCHUMI ILI KUONDOKANA NA UMASKINI


IMG-20170926-WA0035
Na Mwamvua Mwinyi ,Kibaha 

Vijijini MKE wa mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Mkoani Pwani ,Leila Hamoud Jumaa,ameibuka kidedea katika uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti umoja wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi wilayani humo (UWT),kwa kupata kura 176 .

Akitangaza mshindi wa nafasi hiyo ,msimamizi wa uchaguzi huo ,katibu uchumi na fedha wa wilaya ya Bagamoyo ambae pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM ,mkoa wa Pwani,Iddi Swala ,alimtangaza Leila kuwa ni mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho ,akifuatiwa na Fatuma Kisebengo aliyepata kura 19 na Victoria Ngaga kura nne.
Swala ,alisema ,uchaguzi umefanyika kwa uhuru ,uwazi na haki .
Kwa upande wake Leila ,alieleza kuwa ,uchaguzi umepita wagombea na wapambe waondoe tofauti zao ,kwasasa wakaendeleze jumuiya ili kukiimarisha chama .
Alisema ,zoezi la uchaguzi ni la mpito ,kazi kubwa ni kujenga jumuiya kwa ushirikiano .
Leila ,aliwaomba wanawake wilayani humo ,kuondoa migawanyiko kwani haina tija kwao .
Aliwataka wajitambue na kuendelea kupambana kimaendeleo kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali na kufanya shughuli ndogondogo zitakazowaongezea kipato na kuondokana na hali ya umaskini.
“Tuachane na kitabia cha ubinafsi ,wanawake wengi sasa tumeamka tushikane  kwa pamoja kujikomboa kiuchumi ili hali kuondokana na hali ya utegemezi ” alisema Leila .
Alielezea kwamba ,wanawake ni jeshi kubwa ,endapo watashirikiana kwa umoja wao watapiga hatua zaidi na kutoka walipo sasa .
Leila aliwashukuru wajumbe waliopigia kura na ambao hajampigia na kusema hiyo ndio demokrasia .
“Mie sio kama ni bora sana kuliko wenzangu ,la hasha ,lakini naamini uwezo na sifa zangu za kushikana wanawake wenzangu kimaisha ,kwenye shida ,raha ndicho kilichowasukuma mnichague ” alifafanua Leila .
Katika hatua nyingine ,vijana wa UVCCM Kibaha Vijijini, walimchagua Jumanne Mbonde ,kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo wilayani hapo .
Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo ,Omary ambae pia ni mjumbe wa baraza mkoa ,alisema Mbonde ataongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo .
Hata hivyo ,Mbonde alishukuru wajumbe wa uchaguzi huo kwa kumuamini .
Alisema kuchaguliwa kwake haimaanishi wagombea aliogombea nao hawafai hivyo anaomba ushirikiano wao uendelee kwa mustakabali wa kuijenga jumuiya .

No comments