Header Ads

Responsive Ads Here

KUMBUKUMBU MAMA FORTUNATA


PICHA MAMA ROSE
Maisha bila Mama ni magumu naya mateso makubwa; na laiti tungekuwa na uwezo wa kuzuia kifo basi tungezuia kifo chako mama tubaki na wewe, tunakukumbuka mama Fortunata Joseph Msoka. Pengo uliloacha ni kubwa halizibiki. Kwetu ulikuwa zaidi ya mama. Watoto wako tunakukumbuka kwa upendo na malezi bora, bila wewe leo maisha sijui yanyekuwaje. Wajukuu zako wanatamani ungekuwepo leo wakaonja  upendo wa Bibi na kupata simulizi zako.

Leo (18/09/2017) umetimiza miaka minne tangu ulipotuacha, lakini kwetu ni kama jana umetuacha. ulizimika ghafla kama mshumaa uliokuwa unawaka na kutoa matumaini ya mwanga mpya. Unakumbukwa na  Watoto wako wapendwa Paul Msoka, Rose J. Mdami, Constantine Msoka, Jackline Msoka, Wajukuu, Wadogo zako, Shemeji zako, Wifi zako, Wajukuu zako, Wakwe zako, Wanajumuia na majirani zako.  Kwa majonzi makubwa yasiyoelezeka, Mama tuna tumaini na Imani kwamba uko mbinguni na siku moja tutaonana tena, kwa maana maandiko yanasema kila nafsi itaonja mauti 1 Wakorontho:15
Ulitufundisha dini na ukatuonyesha kwa matendo maana ya kumcha Mungu. ndiyo kwa imani hiyo tunamkiri Kristo na kuzidi kukuombea kwa imani tukisimama katika Zaburi ya 147 na Zab 148 inayotutaka kumsifu, kumwabudu, na Kumshukuru Mungu daima kwa ajili yako.  “Mungu akulaze mahali pema mbinguni, Upumzike kwa Amani. Amina”

No comments