Header Ads

Responsive Ads Here

KIM POULSEN KOCHA MPYA WA TIMU ZA TAIFA ZA VIJANA TANZANIA ‘BAKARI SHIME AONDOLEWA’

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limemteua Kim Poulsen kuwa kocha mkuu wa timu zote za vijana  za wavulana zinazosimamiwa na shirikisho hilo zenye umri wa miaka 17 ,20 na 23.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kuwa uteuzi huo umefanywa na uongozi mpya wa shirikisho hilo baada ya kuingia madarakani.
Kabla ya uteuzi huu Kim Poulsen alikua mshauri wa timu z vijana za wavulana ikiwemo Serengeti Boys iliyoshiriki michuano ya fainali za Afrika za vijana zilizofanyika nchini Gabon.
Kwa uteuzi huo wa Poulsen kua kocha mkuu wa timu za vijana inaondoa nafasi ya kocha Bakari Shime ambae awali alikua kocha mkuu wa timu ya Serengeti boys,kwani kwa sasa kocha msaidizi wa timu hiyo ni Osca Mirambo akisaidiwa na Peter Manyika.
Kwa sasa Kocha Bakari Shime anaifundisha timu ya JKT Ruvu iliyoshuka daraja msimu uliopita

No comments