Header Ads

Responsive Ads Here

Katibu Mkuu- Wizara ya Afya Asaini Mkataba na Kampuni ya Neusoft Medical kutoka China


# 1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akimkabidhi mkataba Makamu wa Raisi wa kampuni ya Neusoft  Medical System  Ltd bwana Dan Zhang wakati wa kikao cha kusaini makubaliano na kampuni yake  inayotengeneza vifaa vinavyotumika katika hospitali kilichofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

# 2 (i)
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walioshiriki katika Kikao cha kusaini makubaliano kati ya Wizara ya Afya, na kampuni ya Neusoft  Medical System  wakiongozwa na Katibu Mkuu Dkt. Mpoki Ulisubisya kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
# 3
Makamu wa Raisi wa kampuni ya Neusoft  Medical System  Ltd bwana Dan Zhang akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya  Dkt. Mpoki Ulisubisya katika kikao cha kusaini makubaliano na kampuni hiyo kutoka China inayotengeneza vifaa vinavyotumika katika hospitali, katikati yao ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Afya Tunu Temu.
# 4
Makamu wa Raisi wa kampuni ya Neusoft  Medical System  Ltd bwana Dan Zhang  na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bi. Ying Liu wakipiga makofi kuashiria kufanikiwa kwa makubaliano hayo yaliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya (Hayupo kwenye Picha) katika tukio lililofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
# 5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya na Makamu wa Raisi wa kampuni ya Neusoft  Medical System  Ltd bwana Dan Zhang wakisaini mkataba wa makubaliano baina ya Wizara ya Afya na kampuni ya Neusoft  Medical System  kutoka China inayotengeneza vifaa vinavyotumika katika hospitali , tukio lililofanyika mapema leo Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es salaam.
# 6
Makamu wa Raisi wa kampuni ya Neusoft  Medical System  Ltd bwana Dan Zhang akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya  Dkt. Mpoki Ulisubisya katika kikao cha kusaini makubaliano na kampuni hiyo kutoka China inayotengeneza vifaa vinavyotumika katika hospitali, katikati yao ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Afya Tunu Temu na wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Dorothy Gwajima.


No comments