Header Ads

Responsive Ads Here

KAMPUNI YA UNYWAJI WA KISTAARABU YA TBL YAWAFIKIA WENYE MABAA


UNYWAJI KISTAARABU 1
Meneja Maswala Endelevu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Irene Mutiganzi akizungumza na wahudumu na wateja wa Meeda bar

UNYWAJI KISTAARABU 2
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),John Mtui akizungumza na wahudumu na wateja wa Meeda bar
UNYWAJI KISTAARABU 3
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Patrick Swai akizungumza na wahudumu na wateja wa Soccer Bar
UNYWAJI KISTAARABU 4
Maofisa wa TBL wakiwapiga darasa la unywaji kistaarabu wenye mabaa na wahudumu katika maeneo ya sinza jijini Dar es Salaam
……………………..
Kampuni ya Bia  ya TBL mwishoni mwa wiki iliendesha kampeni ya unywaji kistaarabu kwa wamiliki wa mabaa na wafanyakazi wao lengo kuu likiwa ni kuwapatia elimu hiyo ili waweze kuifikisha kwa watumiaji wa vinywaji vyenye kilevi.
Mbali na kutoa elimu hii ambayo imelenga kufikishwa mikoa yote nchini pia kampuni imeanza kuweka mabango ya kuhamasisha unywaji wa kistaarabu katika maeneo yote vinapouzwa vinywaji.
Akiongea juu ya kampeni hiyo Meneja Mauzo wa TBL,John Mtui,alisema  kuwa unywaji wa kistaarabu ni moja ya ajenda ambayo kampuni imejipanga kuhakikisha inafanikiwa na kuhakikisha watumiaji wa vilevi wanavitumia kwa ajili ya kujenga afya zao na kupata burudani na sio kuleta athari kwenye  jamii na itafanyika nchini kote sambamba na kuwapatia wafanyabishara wanaoshirikiana na kampuni elimu ya ujasiriamali.
Mtui aliongeza kusema kuwa TBL Group kwa muda mrefu imekuwa ikiendesha kampeni za unywaji wa kistaarabu ambazo zimekuwa zikienda sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali za kutokomeza  changamoto ya ajali nchini.”Tumekuwa na kampeni kubwa ya kuhamasisha madereva kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa,semina mbalimbali kuhusu madhara ya ulevi kwa makundi mbalimbali,kutoa elimu ya unywaji wa kistaarabu kwa wadau wetu katika biashara,kuweka nembo kwenye bidhaa zetu kuhusiana na kutowauzia vinywaji vyenye kilevi watoto wenye umri mdogo usioruhusiwa kutumia vinywaji”.Alisema.
Hatua nyingine za kuhamasisha unywaji wa kistaarabu ambazo kampuni imefanikisha alizitaja kuwa ni kuwapatia wafanyakazi mafunzo ya ndani kuhusu madhara ya utumiaji mbaya wa vinywaji vyenye kilevi ambapo hawaruhusiwi kuingia katika maeneo ya kazi wakiwa wametumia vinywaji vyenye kilevi,kuzingatia kanuni za utangazaji wa bidhaa za kampuni zenye kilevi,kushiriki semina na makongamano ya kampeni na kuongelea unywaji wa kistaarabu,
 Alisema  suala la kuhamasisha unywaji kistaarabu liko katika sera ya kampuni ya ‘’Dunia Maridhawa” ambayo inahamasisha kujenga jamii bora sambamba na utunzaji wa mazingira. “Wiki iliyopita tuliadhimisha siku ya unywaji kistaarabu ambayo ilizinduliwa na ABInBev mnamo mwaka 2010 na tunawakaribisha  wadau wote kushirikiana nasi katika kampeni za kuhamasisha unywaji wa kistaarabu na kutuunga mkono kwa kuzingatia matumizi  mazuri ya vinywaji vyetu ili kufanikisha lengo lililokusudiwa’’.Alisisitiza.

No comments