Header Ads

Responsive Ads Here

KAMPUNI YA PANASONIKI YA JAPANI YATOA MSAADA WA TAA ZA SOLA 600


1
Kampuni ya Panasoniki ya Japan imetoa  taa za sola pamoja na chaji zake 600 zilizopokelewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa niaba ya Serikali kupitia Shirika la Maendeleo Duniani -UNDP kwa ajili ya wakazi wanaoizunguka Misitu asilia 12 ya hifadhi inayomilikiwa serikali kuu.

2
Akikaribisha ugeni huo Msaidizi wa shirika la Kimataifa la UNDP, Amon Manyama ,  amesema shirika lao linalenga kuondoa umaskini, Afya Bora na usawa wa Kijinsia , hivyo zoezi hili linalenga kupunguza Umaskini  kwa wananchi wanaozunguka Misitu ya hifadhi na kujenga dhana ya ushirikiano katIka kuhifadhi Misitu hiyo.
Mratibu wa mradi wa Hifadhi wa Misitu asilia hiyo,  Gerald Kamwenda amesema Misitu hiyo asilia kila moja ina asili ndwele ambayo inapatikana katika msitu huo tu. Amesema Msitu wa amani ambao ndiyo mkongwe na wa kwanza kuhifadhiwa una  amfibia aina 3, ndege aina 3, reptilia aina 2 na uufugaji wa vipepeo,
3
Amezitaja hifadhi nyingine kuwa ni Rondo, Mkingu,Nilo,Chome,Magamba, Uluguru, kilombero, Mlima Rungwe, Mlima Hanang, Minziro na Udzungwa ambazo pia zina aina tofauti ya asili zinazovutia.
Kamwenda amesema taa hizo za sola zitaimarisha uhusiano na wakazi wanaozunguka Misitu asilia iliyohifadhiwa.
4
Naye balozi wa Japan nchini,  Masaharu Yoshida amesema  anafurahi kwa sababu nchi yake inaimarisha ushirikiano na nchi ya Tanzania kwa kupitia watanzania wahitaji na watunza mazingira kwa kuwapatia vifaa vya kiteknolojia vinavyorahisisha dhana ya maendeleo ya uchumi kwa jamiijambo ambalo pia linaimarisha ushirikiano wa Kampuni binafsi na serikali.
Akikabidhi Taa hizo Rais wa Panasonic Tanzania Bwana Katshiko Mori amesema Shirika lake linasimamia kaulimbiu inayosema Maisha bora, Dunia bora kwa hiyo wanayo furaha kuyabadilisha maisha ya wakazi wanayozunguka Misitu iliyohifadhiwa , wanaamini wanabadili maisha yao kuwa bora kwa kuwapatia bidhaa zenye ubora wa juu kwa gharama nafuu.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za misitu Profesa dos santos silayo amesema Changamoto inayotukabili mpaka sasa ni nishati ya gharama nafuu ili kupunguza matumizi ya Nishati ya mkaa ambapo mpaka sasa nishati inayotumika mi asilimia 90 inatoka katika Mimea.
Msaada huu ni Muhimu kwa sababu  inawaongezea uwezo wakazi wenye kipato kidogo kutumia nishati rahisi na endelevu ya moto jambo linalopeleka kupunguza matumizi ya nishati itokanayo na Mimea na hivyo kulinda Mazingira na Misitu kwa ujumla.

No comments