Header Ads

Responsive Ads Here

KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI AKAGUA MPAKA KATI YA TANZANIA NA UGANDA MTUKULA MKOANI KAGERA


1
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala  akisalimiana na baadhi ya Maofisa wa Uhamiaji wanaofanya kazi katika Kituo cha Uhamiaji cha Mtukula mkoa wa Kagera alipofanya ziara kukagua Mpaka wa Tanzania na Uganda ili kujionea utekelezaji wa majukumu ya Idara yake  katika Mpaka huo.

2
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala  akikagua Mpaka wa Tanzania na Uganda  katika Kituo cha Mpakani cha Mtukula mkoa wa Kagera, Katikati  ni Kamishna wa Udhibiti wa Mipaka Samuel Magweiga ambaye ameambatana na Dk. Makakala katika ziara hiyo inayolenga kufanya ukaguzi katika Mpaka wa Tanzania na Uganda ili kujionea utekelezaji wa majukumu ya Idara yake  katika Mpaka huo.
3
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala  wa pili kushoto akimsikiliza mmoja kati ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera  alipotembelea kiwanda hicho ili kujionea shughuli za uzalishaji  wa sukari  ambapo alisisitiza dhana ya Uhamiaji na Maendeleo. Dk. Makakala ameambatana na Maafisa mbalimbali wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu.
4
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala  akimsikiliza  Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha Sukari  cha Kagera Bw. REO B.M  alipotembelea Kiwanda hicho. Dk Makakala  amewasisitiza Watendaji Wakuu wa Kiwanda hicho kuhakikisha wanafuata Sheria za Uhamiaji  mara wanapoajiri  wageni kutoka  nje ya nchi. Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Makakala yupo Mkoani Kagera kwa ajili ya kufanya Ukaguzi katika Mpaka wa Tanzania na Uganda ili kujionea utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Uhamiaji.  
5
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala  akimkabidhi kipeperushi chenye taarifa mbalimbali za huduma zinazotolewa na Idara ya Uhamiaji Nchini, Mkuu wa wilaya ya Bukoba aliyepokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera mara baada ya Kamishna Jenerali Dk. Makakala kutembelea Ofisi hiyo akiwa ziarani Mkoa wa Kagera kukagua mpaka wa Tanzania na Uganda.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments