Header Ads

Responsive Ads Here

JUMUIYA YA UMOJA WA VIJANA UVCCM WILAYANI KIBAHA VIJIJINI HATIMAYE IMEPATA SAFU MPYA YA UONGOZI


IMG_3455
Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini Amoud Jumaa ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika mkutano wa uchaguzi mkuu wa Jumuiya ya vijana (UVCCM) Wilaya ya Kibaha vijijini ambao uliofanyika katika ukumbi wa JKT Ruvu Mlandazi, ambapo katika uchaguzi huo  Juma Mbonde alichaguliwa kuwa Mwenyekiti  mpya kwa kupata kura 230 katika ya kura 253 zilizopigwa.

PICHA NA VICTOR MASANGU


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 
JUMUIYA  za  umoja wa vijana (UVCCM)   zimetakiwa kumuunga mkono Rais wa  serikali ya awamu ya tano Dk. John Magufuli katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kuwa wazalendo na nchi yao   ili kuweza  kutimiza azma ya kuwa na Tanzania yenye uchumi wa viwanda na kuwaasa  kuachana kabisa na masuala ya kuwa tegemezi kila kukicha.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa (UVCCM) Mkoa wa Pwani  Ramadhani Kapeto wakati wa mkutano maalumu wa uchaguzi wa jumuiya ya umoja wa vijana katika Wilaya ya Kibaha vijijini ambao umefanyika katika ukumbi wa JKT Ruvu mlandizi.
Katibu huyo alisema kwa sasa vijana hususn wa UVCCM wanatakiwa kubadilika na kuwa na mtazamo chanya wa kujikita zaidi katika kutafuta  fursa zilizopo za  kuanzisha miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo itaweza kuwasaidia kuwapatia kipato ambacho kitaweza kuwasaidia katika kujikimu kimaisha na kupambanana wimbi la umasikini kuliko kukitegemea chama pekee kiwasaidie.
“Vijana hasa wa UVCCM mimi napenda kuwaambia kuwa inabidi kujituma kwa hali na mali kwa lengo la kuweza kukipogania chama chenu, pamoja na kuhakikisha mnakuwa na kazi yoyote ambayo inakuingizia kipato na sio kuwa omba omba hivyo ni vema mkawa na miradi yenu mbali mbali ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa kuliko kukitegemea chama, kazi za chama ni kujitolea hakuna ajira hivyo ni vema mkalifahamu hilo,”alisema Katibu huyo.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini Amoud Juma amewataka vijana  hao wa UVCCM kuhakikisha wanashikamana kwa hali  na mali kwa lengo la kuweza kushinda katika chaguzi mbali mbali na kuweka mipango madhubuti katika kukiimarsiha chama cha mapinduzi kiweze kushinda katika chaguzi  za ngazi  mbali mbali zinazokuja.
Aidha Mbunge huyo ambaye pia ni mlezi wa UVCCM Kibaha vijijini alibainisha kuwa katika kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuwa na uchumi wa viwanda atahakikisha anaweka mipango madhubuti na kuandaa program maalumu  ya kuviwezesha vikundi mbali mbali vya  vijana kwa lengo la kuweza kujikwamua na wimbi la umasikini pamoja na kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
“Kwa upande wangu mimi kama wa jimbo hili la Kibaha vijijini lengo langu kubwa ni kuwasaidia vijana waweze kutimiza malengo yao na kwa sasa nipo katika mipango ya kuendelea kuwawezesha katika vikundi nia na madhumuni ni kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini,”alifafanua Jumaa.
Aidha Mbunge huyo aliongeza kuwa katika kuunga juhudi za Rais wa awamu ya tano atahakikisha kwamba anawapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiliamari pamoja na kuwapatia mitaji  vijana hao ili waweze kuingia katika kufanya biashara pamoja na kuwa na viwanda vidogovidogo ambavyo vitaweza kuwawezesha kujiajiri wao wenyewe.
KATIKA kinyang’anyoro cha uchaguzi  huo wa jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) katika Wilaya ya Kibaha vijijini imeweza kupata safu mpya ya uongozi ambao utaongoza kwa kipindi cha miaka mitano, huku Jumanne Mbonde akichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya baada ya kupata kura 230 kati ya kura 253 ambazo zilipigwa na wajumbe wa mkutano huo kutoka kata 14.

No comments