Header Ads

Responsive Ads Here

JESHI LATOA ENEO LA IHUMWA KWA SERIKALI


1Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene (kushoto mbele) akisaini mkataba na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi wakisaini mkataba wa makadhiano ya eneo ya la Jeshililipo Ihumwa lilikokabidhiwa kwa Serikali kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

2Makabidhiano yakifanyika mbele ya viongozi wa Serikali na wananchi ni aliyekua Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene (kushoto mbele) akikabidhiwa nyaraka za makabhiano na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa makadhiano wa eneo la Ihumwa lenye ukubwa wa Hekta 752.
3Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene (Pili Kulia) akikabidhi nyaraka za makabidhiano ya eneo la Ihumwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana .
4Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene (aliyesimama) akizungumza na viongozi na wananchi wakati wa makadhiano ya lililokuwa eneo la Jeshi Ihumwa.
5Baadhi wa viongozi na walioshiriki kwenye makabidhiano ya lililokuwa eneo la Jeshi Ihumwa.
………………..
Nteghenjwa Hosseah, Tamisemi – Dodoma.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania limekabidhi  eneo la Ekari 1,855 sawa na Hekta 752 lililopo kwenye Kambi ya Ihumwa Mkoani Dodoma kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene ili liweze kutumika kwa ujenzi wa Ofisi za Serikali.
Akikabidhi eneo na nyaraka zinazohusika Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Hussein Mwinyi amesema eneo linalokabidhiws limegawanyika katika ameneo makuu matatu  ambayo ni eneo Na.4 lenye ukubwa  wa Ekari 699.9 ambalo ndio eneo halali la Jeshi na Nyaraka za Uthamini kwa ajili ya eneo Na.5 ambalo bado halijalipwa Fidia ya Tsh Bil 1.4 kwa wananchi wa kijiji cha Mtuma.
Pia aliongeza kuwa makabdhiano hayo pia yanahusisha Nyaraka za uthamini wa eneo Na. 2 lenye ukubwa wa Ekari 304 ambalo bado halijalipwa Fidia ya Tsh Mil 866 kwa wananchi wa Kijiji cha Mahoma Makulu.
Amesisitiza kuwa baada ya makabidhiano haya Mamlaka zinazohusika zichukue jukumu la kupima upya Eneo la Jeshi, eneo la barabara na eneo linalokabidhiwa ili kubainisha na kuweka  mipaka halisi ya kila eneo.
Akipokea eneo na nyaraka hizo aliyekuwa Waziri wa Tamisemi Mhe. Simbachawene ameshukuru Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa uamuzi wa kizalendo wa kutoa eneo hilo kwa maslahi mapana ya Serikali na Wananchi kwa ujumla.
“Eneo hili tunalolipokea leo  litasaidia sana  wakati huu ambao Serikali inahamia Dodoma na inahitaji maeneo kwa ajili ya  matumizi mbalimbali  ya Serikali hivyo uongozi wa Mkoa pamoja na Halmashauri msimamie ipasavyo ili malengo tuliyojiweka yaweze kufikiwa kwa haraka na ufanisi wa hali ya juu” Alisema Mhe. Simbachawene.
Pia aliwaagiza viongozi wa Manispaa ya Dodoma waingilie kati na kudhibiti uuzaji holela wa maeneo katika Mji wa Dodoma unaokua kwa kasi ili kuzuia migogoro kati ya Serikali na Wananchi lakini pia wananchi na wananchi inayoweza kujitokea hapo baadae.
“Nimekuwa nikishuhudia na kuona watu kutoka maeneo ya mbali wakija kununua viwanja na mashamba makubwa katika Mji wa Dodoma naomba msimamie hili kwa sababu maeneo mengine yamekwisha fanyiwa uthamini na wamiliki kulipwa Fidia lakini kwa sababu bado hakujaendelezwa wananchi wale wanauza tena maeneo hayo kwa watu wengine hii inaweza kuleta athari kubwa hapo baadae”
Aliyekuwa Waziri wa Tamisemi Mhe. Simbachawene amekabdhi eneo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordani Rugimbana ambaye naye alikabidhi kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma Mhe.Prof. Davis Mwamfupe sambama na Mkurugenzi Ndg.Godwin Kunambi.

No comments