Header Ads

Responsive Ads Here

HOTUBA YA MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA KWA WANANCHI WA DAR ES SALAAM HII HAPA


index
Watumishi wa Manispaa zote, idara za AFYA(wauguzi, madaktari, maafisa afya), ELIMU (walimu Shule za Msingi, na sekondari, waratibu wa elimu kuanzia kata, wilaya na Mkoa,  
-Askari wa Vikosi vyote Jeshi la Polisi(kanda maalum, mikoa ya Kipolisi temeke, kinondoni, ilala, Ubungo, kigamboni, na wilaya zake), Magereza, na uhamiaji, Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ na kikosi cha Zima moto

DONDOO MUHIMU ZA HOTUBA
Kila MTUMISHI anaefanyakazi kazi Chini ya Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam KUPEWA kiwanja cha UJENZI WA MAKAZI YA KUDUMU kwa Gharama ya Square Mita moja kwa shilingi elfu nne (4,000 Tsh) badala ya square Mita moja kwa Shilingi elfu kumi na Tano (15,000 Tsh)
-Malipo Ndani ya Miaka Mitano (5) Mtumishi Ruksa Kujenga na Kulipa taratibu Ndani ya Miaka mitano.
-Vibali vya Ujenzi BURE uku Mkipewa KIPAUMBELE.
Ndugu zangu WATUMISHI, nikiwa Msaidizi wa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, dkt. John Magufuli amenipa Dhamana ya Kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam, mimi na timu yangu tutaendelea kushughulika na kutatua changamoto mbalimbali ambapo natambua ziko changamoto za Kimazingira zinazowagusa wafanyakazi mfano Sekta ya afya kutokuwa na wodi za kulaza Wagonjwa, upande wa Polisi kutokuwa na vitendea kazi mfano magari ya kutosha, upande wa Walimu kutokuwa na ofisi, upande wa michezo kutokuwa na viwanja vya michezo.
Kwa upande wa wananchi tumeona masuala ya migogoro ya Ardhi, haya yote ni Majukumu yetu sisi kama viongozi na wawakilishi wa Rais ambae alitoa ahadi wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 ambapo wananchi walimpa ridhaa ya kuliongoza taifa hili kama Rais wao na amiri Jeshi mkuu.
Ndugu zangu WATUMISHI, natambua ziko changamoto zinazowahusu watendaji wetu, ni kweli tutajenga WODI, tutajenga OFISI, ni kweli tutaleta magari ya polisi lakini swali bado litabaki mtumishi huyu wa kawaida alieko kwenye sekta ya afya ambae hana muda wa kufanya kasi zingine za kujiongezea kipato kutokana na kutokuwa na Muda, je maisha yake na kipato chase yanampa matumaini na MORARI ya kufanya kazi kwa ufanisi? mwalimu ambae anaangaika na watoto wetu ili wafaulu vizuri kuanzia asubuhi mpaka jioni na kusahihisha madaftari yao na hapo hapo anatakiwa kuandaa somo la kesho, hivi atapata atapata muda wa kufanya Biashara ya KARANGA na kupata faida?
Hebu tafakari Askari polisi wetu polisi wa nafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha usalama utakuwepo katika mkoa, Hebu tafakari Muuguzi ambae ni MKUNGA analazimika kukesha KUZALISHA wake zetu na kutunza vichanga vyetu hivi huyu anapata Muda Gani wa kufanya biashara?
Hata kama wakichukua MIKOPO katika taasisi mbalimbali wanajikuta wanashindwa Kurejesha kwa sababu biashara zao zinasimamiwa na Ndugu ambao hawana UZOEFU wanajikuta biashara zinakufa na wanapata mzigo mkubwa wa KULIPA MADENI kwa riba kubwa sana na kujikuta MITAJI imekata haya ni maswali magumu kwangu kuyajibu, kwani hata akitoka nje kwenda kuuziwa bidhaa atanunua kwa bei ya soko Hatauzwi kwa bei ya chini kwa kuwa yeye ni mwalimu, au polisi au muuguzi, atauziwa sawa na mfano wa mfanyabiashara Biashara, mwanasiasa atauziwa bei moja tu licha ya kuwa hawa watu wawili wanatofautiana kipato na aina ya kazi ila wanauziwa bei sawa hii sio sawa kwa Watumishi wangu.
Ndugu zangu WATUMISHI, kutokana na sababu hizo na nyingine nyingi, nimeona mimi kama msaidizi wa Mhe, Rais, dkt. John Magufuli iko HAJA na TIJA kuanza sasa na KUGUSA na maisha ya watendaji Mmoja mmoja na kumpa FAHARI ya yeye kama Mwalimu, muuguzi au polisi ili anaporejea nyumbani mtoto wake nae atamani kuwa Mwalimu au Muuguzi, au Daktari kwa sababu anaona FAHARI mzazi wake anayopewa katika utumishi wake kwa wananchi.
Ndugu zangu WATUMISHI, nimetafakari na kufikiria sana katika njia sahihi ya KUWAKOMBOA Watumishi hawa na kwa kuanzia na kuwapatia VIWANJA VYA KUJENGA NYUMBA ZA KUISHI (makazi), katika utekelezaji wa jambo hili Nimefanya mazungumzo na WADAU mbalimbali pamoja na WAPIMAJI wakubwa wa viwanja, kuangalia Bei ya SOKO ambayo inatofautina, mana natambua yako maeneo yanauzwa viwanja vilivyopimwa kwa Gharama ya Elfu ishirini na tano (25,000) kwa Square Mita moja na bei ya soko inakwenda mpaka shilingi elfu kumi na mbili (12,000) kwa square Mita moja. Hatua hii imesababisha Watumishi wengi kushindwa kumudu kununua Viwanja katika maeneo mazuri yaliyopimwa Hatua ambayo imesababisha baadhi yao kujenga nyumba katika maeneo yasiyostahili na kujikuta WANABOMOLEWA.
Ndugu zangu WATUMISHI, NAOMBA NITANGAZE RASMI KWA WATUMISHI WANGU KUWA NIMEFANIKIWA KUWASHAWISHI WATU WENYE MAENEO MAKUBWA NA WAPIMAJI WAKUBWA WA VIWANJA NA KUFANIKIWA KUFANYA MAJADILIANO NAO KWA KINA NA KUPATA VIWANJA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YALIVYOPIMWA AMBAVYO VITAUZWA KWA SQUARE MITA MOJA SHILINGI ELFU NNE TU (4,000 Tsh) badala ya shilingi elfu kumi na tano (15,000 Tsh) kwa Square Mita.
Ndugu zangu WATUMISHI, viwanja hivi VIPO TAYARI KWA AJILI YENU na tayari nimeshaelekeza Viongozi wenu Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es salama, Afisa Uhamiaji wa Mkoa,Afisa Magereza wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa, Afisa ELIMU mkuu wa mkoa, Wakurugenzi wote wa Manispaa, wakuu wa wilaya KUWAELEZA Watumishi wao na kuwakutanisha Watumishi wao na WAHUSIKA WA viwanja hivyo kwa ajili ya kuanza UTEKELEZAJI.
Ndugu zangu WATUMISHI, pamoja na kuuziwa viwanjwa hivyo kwa Square Mita moja kwa shilingi elfu nne, Mhe Makonda pia AMEAGIZA kama Mtumishi Hana Fedha za Kulipa kwa wakati mmoja APEWE muda wa Kulipa ndani ya miaka mitano (5), ambapo amesema endapo Mtumishi atahitaji kuanza ujenzi kabla ya kukamilisha MALIPO Mhe Makonda AMEELEKEZA mtumishi huyo ARUHUSIWE kuendelea na Ujenzi na Atalipa taratibu taratibu uku akiendelea na Ujenzi.
Mwisho Mhe Makonda AMEWAELEKEZA Wakurugenzi wa Manispaa ZOTE katika Mkoa wa Dar es Salaam kuwapa KIPAUMBELE katika utoaji wa VIBALI (bure) vya Ujenzi wa Makazi ya Kudumu pasipo kutoa FEDHA yoyote.
Mhe Makonda amesema LENGO na NIA ya serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam ni kuleta HESHIMA na kutoa UTUMISHI iliotukuka kwa Watumishi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam Chini ya Uongozi wa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa Mhe, dkt. John Magufuli.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Dar es Salaam, Mungu Mbariki na Kumlinda Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

No comments