Header Ads

Responsive Ads Here

GAMBO AWAAGIZA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA UMOJA ILI WAACHE ALAMA


rc 1

Na Mahmoud Ahmad Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewaagiza watumishi wote wa halmashauri ya wilaya ya Arusha kufanya kazi kwa weledi na umoja ili waache alama ambayo itakumbukwa na wananchi wanaowahudumia.

Gambo aliyasema hayo mapema leo hii alipokuwa akizungumza na viongozi,na watumishi wa halmashauri hiyo ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara  siku tano ya kutembelea miradi na kuongea na wananchi ikiwa ni   mwendelezo wa  ziara yake aliyokuwa nayo ya kutembelea halmashauri zote za mkoa wa arusha.
Alisema kuwa watumishi ni viongozi ambao wamepewa dhamana kubwa ya kuwaongoza wananchi na hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa weledi huku wakihakikisha kuwa wanafuata kanuni,sheria na taratibu ili waweze kuacha alama ambayo daima wananchi wataikumbuka pindi watakapoacha utumishi wao.
Vile vile aliwaagiza maafisa kilimo wa halmashauri hiyo kutoka maofisini na kuhakikisha kuwa wanaenda kutoa huduma za kitaalamu  kwa wanachi walioko vijijini kwani wapo wakulima wanaolalamika kutoonekana kwa maafisa kilimo hivyo kukosa utaalamu wa kilimo.
Hata hivyo gambo amewasihi  watumishi wote  wanaokabiliwa na changamoto ya kutopanda madaraja,na malimbikizo ya mishahara waendelee kuchapa kazi na kuwa wavumilivu kwani serikali inaelewa changamoto hizo na kwamba changamoto hizo zimetokana na uhakiki wa watumishi pamoja vyeti feki na taratibu zikishamakizika wataanza kulipwa staiki zao zote.
Awali mkurugenzi wa halmashauri hiyo dt Wilson Mahera akisoma hotuba yake alisema kuwa katika halmashauri hiyo wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa wafanyakazi hivyo kuathiri utoaji huduma kwa wananchi ambapo changamoto hiyo inatokana na wale wote waliokuwa wakitumia vyeti feki katika halmashuri hiyo.

No comments