Header Ads

Responsive Ads Here

FAHAMU YALIYOJIRI ZIARA YA DC HAPI KINONDONI TAR 28/9/2017


index
*Mkuu wa wilaya alisimama kuzungumza na wafanyabiashara wa barabarani ambapo waliomba eneo/nafasi sokoni ili waondoke barabarani wanakofanyia biashara.

*Wafanyabiashara waeleza juu ya eneo la kiwanja cha soko kinachodaiwa kupewa mtu binafsi na kujenga shule binafsi.
*DC Hapi ameagiza Mkurugenzi kumpatia taarifa juu ya kiwanja hicho na kumtaka mmiliki wake kufika kwake akiwa na nyaraka zote za umiliki.
*Aidha DC amewataka wafa
Wafanyabiashara hao kwenda kwenye soko la Bunju B ambako kuna nafasi.
BUNJU B SOKONI
*DC Hapi amezindua choo cha kisasa cha soko kilichojengwa na manispaa ya Kinondoni kama sehemu ya uboreshaji wa soko hilo.
*Choo hicho kina matundu 12, 7 ya wanawake, 5 wanaume, mabafu mawili, vyumba viwili vya walemavu na sehemu 7 za haja ndogo kwa wanaume (urinals).
*DC amekagua ujenzi wa machinjio ya kisasa unaoendelea sokoni hapo itakayokua na uwezo wa kuandaa kuku zaidi ya 1500 kwa siku.
*Maboresho yaliyofanyika sokoni hapo ni kujengwa Choo, machinjio, huduma ya maji na umeme na kuhakikisha daladala zinapita sehemu iliyotengwa sokoni.
BUNJU B MKUTANO
*DC Hapi amefanya mkutano wa hadhara kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
*Mkuu wa wilaya amewataka wafanyabiashara wanaofanya biashara barabarani kinyume cha sheria kuhamia sokoni ndani ya siku 14, kwani hoja zao zote walizotoa zimefanyiwa kazi na maboresho yamefanyika na yanaendelea kufanyika sokoni.
*DC Hapi amemtaka Mkurugenzi wa manispaa, RPC, uongozi wa soko na wafanyabiashara hao kukaa pamoja na kutekeleza agizo hilo kwa wakati.

No comments