Header Ads

Responsive Ads Here

DK.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM CCM ZBAR


DSC_5802
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa  Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,


Is-haka Omar, Zanzibar.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, leo amekiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM  Taifa Zanzibar.
Kikao hicho cha kawaida kimefanyika kwa mafanikio makubwa katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar Ndg Waride Bakari Jabu, pamoja na mambo mengine  kilipokea  na kujadili majina ya wagombea 50 waliojitokeza  kuomba nafasi za Uenyeviti  CCM  Wilaya 12 za Unguja na Pemba na kutoa mapendekezo yake ili  kuyapeleka  katika vikao husika.
Aidha  kikao hicho kilimpongeza  Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kufanya ziara ya Chama na Serikali kwa wakati mmoja kufuatilia Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 Unguja na Pemba kwa mafanikio makubwa  .
Kwa upande wake Rais za Zanzibar aliwashukuru viongozi, watendaji na  wananchi mbalimbali walioshiriki katika ziara  yake na kusisitiza juu ya umuhimu wa viongozi wa Chama na Serikali kuteremka chini  kwa wananchi  na kushirikiana nao katika harakati za  maendeleo kubaini changamoto zilizopo na kazipatia ufumbuzi .
Dk Sheni alimalizia kwa kusema viongozi wa Chama na Serikali wana wajibu mkubwa wa kutimiza wajibu wao  kikamilifu katika kukiwezesha Chama na Serikali kuendelea kukubalika zaidi kwa  wananchi na kushinda kwa kiwango cha juu zaidi  katika uchaguzi mkuu ujao.

No comments