Header Ads

Responsive Ads Here

Bomu la Korea Kaskazini: Tunayoyajua kufikia sasa


Mapema Jumapili, shirika la habari la taifa la Korea Kaskazini lilitoa picha ambayo ilidaiwa kuwa ya kiongozi wan chi hiyo Kim Jong-un akisimamia bomu la haidrojeni

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMapema Jumapili, shirika la habari la taifa la Korea Kaskazini lilitoa picha ambayo ilidaiwa kuwa ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un akisimamia bomu la haidrojeni
Korea Kaskazini imetangaza kwamba imefanikiwa kufanya majaribio ya bomu la haidrojeni - aina ya bomu la nyuklia.
Haya hapa ndiyo mambo tunayoyafahamu kufikia sasa:
Korea Kaskazini imesema jaribio hilo la kulipua bomu "limefanikiwa kabisa".
Runinga ya taifa ya Korea Kaskazini imetangaza kwamba bomu hilo linaweza kuwekwa kwenye kombora, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Trump na Abe wazungumza
Shirika la habari la Japan NHK, linasema kuwa waziri mkuu Shinzo Abe na rais wa Marekani Donald Trump, wamezungumza kwa njia ya simu. Walikubaliana kushirikiana na Korea Kusini kuiongezea shinikizo Korea Kaskazini, shirika hilo liliongeza kusema.
NHK ilisema kuwa Bwana Abe anataka kutathmini taarifa kadhaa anazopokea, kujadili nia mwafaka na nchi zingine na kuchukua hatua kulinda maisha na mali.
Trump na Abe wazungumzaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTrump na Abe wazungumza
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe ameghadhabishwa na jaribio hilo ambalo lilisikika kama mitetemeko ya ardhi nchini mwake. Amesema "haikubaliki kamwe",
Mabomu ya Haidrojeni ndiyo yenye nguvu zaidi kuwahi kuundwa duniani. Ni ya nyuklia lakini huwa na tofauti kidogo na mabomu ya atomiki.Haki miliki ya pichaKCNA
Image captionMabomu ya Haidrojeni ndiyo yenye nguvu zaidi kuwahi kuundwa duniani. Ni ya nyuklia lakini huwa na tofauti kidogo na mabomu ya atomiki.
Mitetemeko miwili ya ardhi
Maafisa wa Japan wamethibitisha kwamba mitetemeko ya ardhi iliyosikika ikitokea upande wa Korea Kaskazini ilisababishwa na mlipuko wa bomu la nyuklia. Akiongea baada ya mkutano wa Baraza la Taifa la Usalama la Japan, Waziri wa Mambo ya Nje Taro Kono amesema: "Baada ya kutathmini data tumethibtiisha kwamba lilikuwa jaribio la bomu la nyuklia." Maafisa wa Japan wamesema tetemeko la ardhi la nguvu ya 6.3 katika vipimo vya Richter lilitokea Korea Kaskazini kutokana na mlipuko huo.
Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema imetuma zaidi ya ndege tatu za kivita kutoka kambi zake Japan kwenda kuchukua vipimo vya viwango vya miali nururishi.
Mitetemeko ya ardhi ilitokea upande wa Punggye-ri, eneo ambalo Korea Kaskazini imekuwa ikitumia kufanyia majaribio silaha za nyuklia.
Mitetemeko ya ardhi ilitokea upande wa Punggye-ri, eneo ambalo Korea Kaskazini imekuwa ikitumia kufanyia majaribio silaha za nyuklia.Haki miliki ya pichaALAMY
Image captionMitetemeko ya ardhi ilitokea upande wa Punggye-ri, eneo ambalo Korea Kaskazini imekuwa ikitumia kufanyia majaribio silaha za nyuklia.
Idara ya Jiolojia ya Marekani (USGS) imethibitisha kuwa tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 6.3 na lilitokea takriban kilomita 22 kutoka Sungjibaegam. Walikuwa awali wamesema llikuwa na nguvu ya 5.6 lakini baadaye wakabadilisha hadi 6.3.
USGS wameongeza kwamba lilisababishwa na mlipuko ingawa hawakusema kama lilitokana na mlipuko wa nyuklia.
Kituo cha kufuatilia mitetemeko ya ardhi cha China (CENC) kimesema kwamba kulitokea tetemeko la pili katika eneo karibu sawa na palipotokea tetemeko la kwanza, takriban dakika nane baada ya mlipuko wa kwanza.
Kituo hicho kilisema mlipuko wa pili ulitokea mwendo wa saa 11:38 mjini Beijing, ambazo ni sawa na saa kumi na mbili na dakika 38 Afrika Mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Taro KonoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWaziri wa Mambo ya Nje wa Japan Taro Kono
Kituo hicho kimesema tetemeko la pili lilikuwa na nguvu ya 4.6, na linaaminika lilitokana na kuporomoka kwa njia ya chini kwa chini iliyotumiwa kulipulia bomu hilo. USGS pia wamethibitisha kutokea kwa tetemeko la pili.
Mtaalamu wa silaha Melissa Hanham ameambia BBC kwamba hali kuwa USGS wamerekebisha makadirio yao ya nguvu la tetemeko kutoka 5.6 hadi 6.3 ni ishara ya nguvu za mlipuko ulitokea.
Katika kipindi cha mwongo mmoja, Korea Kaskazini imefanikiwa kongeza nguvu za milipuko yake ya nyuklia kutoka 4.3 mwaka 2006 hadi 6.3 leo.
Hilo likithibitishwa, mlipuko huo utakuwa ndio wa nguvu zaidi kuwahi kulipuliwa na Korea Kaskazini.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa la Japan limesema mitetemeko iliyotokea ilikuwa na nguvu karibu zaidi ya mara kumi ya milipuko iliyotokea awali Korea Kaskazini.
Idara ya Jiolojia ya Marekani (USGS) imethibitisha kuwa tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 6.3 na lilitokea takriban kilomita 22 kutoka SungjibaegamHaki miliki ya pichaUSGS
Image captionIdara ya Jiolojia ya Marekani (USGS) imethibitisha kuwa tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 6.3 na lilitokea takriban kilomita 22 kutoka Sungjibaegam
Korea Kusini yawasiliana na Marekani
Korea Kusini imesema maafisa wake wa ngazi ya juu wa usalama wamewasiliana na Marekani kuhusu hatua ambazo wanafaa kuchukua.
Shirika la habari la serikali la Yonhap limesema Mkuu wa Shirika la Taifa la Usalama Chung Eui-yong amefanya mazungumzo ya dakika 20 kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani, Mshauri Mkuu wa Masuala ya usalama HR McMaster muda mfupi baada ya Korea Kaskazini kutangaza kufanya jaribio la bomu la Haidrojeni.
China yashutumu jaribio
Wizara ya mambo ya nje ya China imetoa taarifa ikisema "inapinga vikali" na "kushutumu vikali" jaribio la bomu la nyuklia lililofanywa na Korea Kaskazini. China ni jirani na mshirika mkuu wa Pyongyang.
Silaha kubwa
Mchanganuzi wa masuala ya silaha amesema mitetemeko iliyosikika ikitokea Korea Kaskazini ilikuwa mikubwa sana, iwapo ilitokana na silaha ya nyuklia.
Bruce Bennett kutoka shirika la Rand Corporation amesema mitetemeko ya nguvu ya 6.3 ni ishara kwamba ilikuwa "silaha kubwa"
Ameongeza kuwa: "Iwapo si silaha kamili ya haidrojeni, basi inakaribia sana bomu la aina hilo kuliko kitu kingine chochote kilichowahi kulipuliwa awali."
Kim Jong-un akiwa na bomu
Mapema Jumapili, shirika la habari la taifa la Korea Kaskazini lilitoa picha ambayo ilidaiwa kuwa ya kiongozi wan chi hiyo Kim Jong-un akisimamia bomu la haidrojeni likiwekwa kwenye kombora ambalo linaweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.
Bomu hatari zaidi kuwahi kuundwa
Mabomu ya Haidrojeni ndiyo yenye nguvu zaidi kuwahi kuundwa duniani. Ni ya nyuklia lakini huwa na tofauti kidogo na mabomu ya atomiki.
Bomu la Haidrojeni kutoa nishati yake kutokana na kuunganishwa kwa atomu mbili ilhali la atomiki hutokana na kupasuliwa kwa atomu.
Korea Kaskazini imewahi kudai kuwa imefanyia majaribio bomu la Haidrojeni awali, Oktoba mwaka jana, lakini madai hayo hayakuthibitishwa.
"Bomu la kawaida la nyuklia huwa na nguvu sawa na mlipuko wa tani 10,000 za TNT, na mabomu haya ya Haidrojeni huwa na nguvu zadii ya mara 10 ya bomu la kawaida," anasema Paddy Regan, profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Surrey.
Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imesema nguvu za mlipuko huo zilikuwa sawa na kilotani 100.
Profesa wa sayansi ya saisa katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Massachusetts (MIT) cha Marekani Vipin Narang amesema hiyo itakuwa hatua kubwa sana iliyopigwa na Pyongyang katika kuzuia maadui kushambilia kwa sababu bomu kama hilo linaweza kuangamiza jiji.
Ukilinganisha na bomu la Nagasaki?
Makadirio ya awali yanaonesha bomu hilo la Korea Kaskazini - kwa kuzingatia nguvu za mitetemeko - lilikuwa na mlipuko wa nguvu ya kilotani 100.
Bomu lililoangushwa na Marekani katika mji wa Nagasaki, Japan mwezi Agosti mwaka 1945 lilikuwa na nguvu ya kilotani 20.
Bomu hilo la Nagasaki liliua watu 70,000 papo hapo.
Bomu hilo la Nagasaki liliua watu 70,000 papo hapo.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBomu hilo la Nagasaki liliua watu 70,000 papo hapo.
Mitetemeko yasikika Urusi
Raia wa Urusi wanaoishi katika mji wa mashariki mwa nchi hiyo wa Vladivostok wanasema waliisikia mitetemeko iliyotokea kutoka Korea Kaskazini. Shirika la habari la Primamedia limeripoti kuwa mitetemeko hiyo ilisikika kusini magharibi mwa eneo la Primorsky.
Mataifa yamesema nini?
Hivi ndivyo nchi mbalimbali zilivyopokea na kuchukua hatua baada ya taarifa kwamba Korea Kaskazini imefanya jaribio la sita la nyuklia:
• Korea Kusini imeitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la Usalama
• Waziri wa mambo ya nje wa Japan Taro Aso ameshutumu jaribio hilo kwa maneno makali zaidi na kusema ni ukiukaji wa maazimio ya Umoja wa Mataifa ambao hauwezi kusameheka.
• Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema jaribio jingine la nyuklia "haliwezi kukubalika kamwe".
Mwanamke maarufu Korea Kaskazini
Tangazo la jaribio hilo la nyuklia katika runinga ya taifa ya Korea Kaskazini lilifanywa na mwanamke mtangazaji maarufu zaidi nchini humo Ri Chun-hee.
Amelia, akacheka na kupiga kelele akitoa matangazo mbalimbali makuu kutoka kwa serikali ya Korea Kaskazini kwa kipindi cha miaka 40.
Tangazo la jaribio hilo la nyuklia katika runinga ya taifa ya Korea Kaskazini lilifanywa na mwanamke mtangazaji maarufu zaidi nchini humo Ri Chun-heeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTangazo la jaribio hilo la nyuklia katika runinga ya taifa ya Korea Kaskazini lilifanywa na mwanamke mtangazaji maarufu zaidi nchini humo Ri Chun-hee

No comments