Header Ads

Responsive Ads Here

BODI YA UTALII YAKABIDHI BENDERA KWA MWANAMITINDO WA MAVAZI YA KIUTAMADUNI


DSC03689
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi Devota Mdachi amemkabidhi Mwanamitindo Joctan Makeke bendera ya Tanzania ili aweze kuipeperusha katika jukwaa la mashindano ya “Face of Culture” yanayotarajiwa kufanyika Septemba 9, 2017 nchini Nigeria. Katika Mashindano hayo yatakayohusisha makundi mbalimbali, Joctan ambaye ni mwanamitindo pekee aliyepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika kundi la mavazi ya kiutamaduni.

Wakati wa makabidhiano hayo, Bodi pia imempatia mwanamitindo huyo vipeperushi vinavyotangaza Utalii wa Tanzania kwa lengo la kuwahamasisha washiriki wengine Kutoka nchi mbalimbali kuja kuvitembelea vivutio vya utalii vya Tanzania.

No comments