Header Ads

Responsive Ads Here

BODI YA RUFAA YAWAKOA WANAFUNZI 37 WA MILAMBO WALIOKUWA WAMEFUKUZWA


Na Mwandishi wetu.
RS –TABORA
WANAFUNZI 37 wa Shule ya Sekondari ya Milambo ambao walikuwa wamefukuzwa kwa kosa la kutoroka na kutokuwepo kwa maeneo ya Shule Usiku wamesamehewa na BODI ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora na kutakiwa kutafuta Shule nyingine za kuhamia.


Akisoma mapitio ya rufaa zao jana mjini Tabora , Mwenyekiti wa Bodi ya Rufaa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa kutokana na maelezo ya wanafunzi na wazazi waliona kuwa Bodi ya Shule ya Sekondari Milambo ilikuwa sahahi kuwafukuza.

Alisema kuwa Bodi ya Rufaa ilifikia uamuzi huo wa kuwasaheme baada  wanafunzi na wazazi wao kukiri makosa na kuomba msamaha na kufanya majadiliano na kwa mawasiliano ya karibu na ile ya Shule ndipo walioamua kuwasaheme kwa masharti ya kuwa wahamie sehemu nyingine ili wamalizie masomo yao.

Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Rufaa alisema kuwa baada ya msamaha huo wanafunzi hao hawataruhusiwa kurudi Milambo badala yake wazazi na wanafunzi hao watalazimika kutafuta Shule za kuhamia ambao uongozi wa Mkoa na ule wa Shule utawasaidia kuwaandika barua na kuwajazia fomu zitakazohitajika.

Alisema kuwa ni vema katika Shule watakazohamia wakawa mabaolozi wazuri kwa watiifu wa sheria na taratibu zinazongoza mfumo wa kujifunza na kupata elimu na masiha ya jumla ya shule.
Aidha Mwanri alitoa angalizo kwa wanafunzi wa Shule nyingine wasije wakafanya makosa na kisha kukimbilia Ofisi kwake kwa nia ya kukata rufaa , kwani alatazimika kufukuzwa na kuongeza kuwa huo ndio msamaha wa mwisho.
Naye Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tabora anayeshughulikia Elimu Suzana Nussu aliwaomba vijana hao ambapo wamepata msahama huo wa Bodi kufuata mambo ambayo yamewapeleka Shuleni ili waweze kumaliza bila matatizo.
Alisema kuwa licha ya kuwa watapata uhamisho kwenda Shule mbalimbali ,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itaendelea kufuatilia tabia zao popote watakapokwenda ili kuona kama wanatii sheria na taratibu.
Mzazi mmoja wa Wanafunzi hao Hamis Magazi aliishukuru Bodi ya Rufaa na ile ya Shule kwa hatua hiyo na kuwataka wanafunzi hao waliosamehewa kutorudia tena makosa hayo kwani ikitokea tena hawatakuwa na sehemu nyingine ya kukimbilia.
Alisema kuwa ni hekima ya viongozi wote wa Bodi ya Shule na Bodi ya Rufaa kuamua kuwa wasaemehewe vinginevyo wangeweza hata kukataa kukaa nao meza moja.
Mmoja wa wanafunzi wa Kidato cha Sita anayechukua masomo ya Uchumi, Jiografia na Hisabati(EGM) Ally Ramadhani akiri kwa niaba ya  wenzake kufanya makosa hayo na kuahidi kuwa mabolozi wazuri katika shule za Sekondari watakazohamia kwa ajili ya kumalizia masomo yao.
Kundi la wanafunzi waliosamehewa ni tofauti na wale wa shule hiyo wanatuhumiwa kutoroka usiku na kwenda maeneo ya jirani na shule na kuvamia sherehe ya mkazi mmoja wa Tabora na kusababisha fujo zilizosababisha baadhi yao kujeruhimwa ambapo 21 wameshafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilayani Tabora mjini na kusomewa mashtaka 12.

No comments