Header Ads

Responsive Ads Here

BARAZA MAALUM LA HALMASHAURI MBILI ZA MJI WA GEITA NA WILAYA MKOANI GEITA ZIMETANGAZA MGOGORO NA MGODI WA GGM


Wajumbe ambao ni madiwani wa halmashauri mbili ya Mji na Wilaya ya Geita pamoja na watumishi mbali mbali wakifuatilia kikao taarifa na maadhimio juu ya kikao ambacho kinaendelea.


Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati za ulinzi na usalama akielezea juu ya hatua hizo ambazo zimechukuliwa na mabaraza hayo.

Mbunge wa Geita ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Joseph Kasheku Msukuma,akielezea na kuunga hoja ambayo imetolewa na wajumbe.

Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji wa Geita ,Akisoma taarifa na maadhimio juu ya Mgodi wa GGM.

Baraza maalum la madiwani lililojumuisha Madiwani wa Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Geita limesema hawako tayari kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa Geita, GGM hadi mgodi utakapokuwa tayari kuwalipa Dola 12,645,345. 

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa madai yatokanayo na kodi ya huduma kutoka mgodi wa dhahabu wa GGM, madai ya kuanzia mwaka 2004 hadi 2013.

Hali hiyo imesababisha madiwani wa Halmashauri zote mbili kukutana kwenye kikao ambacho kimewahusisha watendaji wa halmashauri zote, wananchi na afisa kutoka mgodi wa GGM na kuutaka mgodi huo kusitisha huduma za jamii ambazo  walikuwa wakizifanya pamoja na magari ya kampuni hiyo kutotumia barabara za Halmashauri hizo pamoja na kuzuia huduma ya maji kufika kwenye mgodi huo. 

Magulu Kuzenza ambaye ni diwani wa kata ya Bukondo, Elias Ukumu Diwani wa Nyachiluluma na Bi Amina Swedi Kanijo wameeleza kuwa hawawezi kuendelea kuubembeleza mgodi huo 

Akisoma taarifa ya kamati ya Mkuu wa Mkoa ya wafanyabiashara Kaimu Mwenyekiti wa TCCIA John Luhemeja ameelezea mapendekezo ya kamati hiyo juu ya namna ambavyo wamewaza kubaini ujuma ambazo zinafanywa na mgodi huo. 

“Tumefatilia tukabahini kuwa kuna ujuma ambazo zimeendelea kufanywa na baadhi ya watendaji wa mgodi wa GGM kwa kushindwa kutoa fursa za ajira kwa maeneo haya na mwisho wa siku kujikuta wanatoa ajira kwa  watu wa kanda ya kasikazini ikiwemo swala la tenda hivyo tunaamini tamko letu la leo litatoa mstakabari juu ya mambo ambayo yanafanywa na mgodi”Alisema Luhemeja
 
Kutokana na mapendekezo ambayo yametolewa ya mgodi kutokupitisha magari yake kwenye Halmashauri hizo  Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama Wilayani Humo ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo,Mwl Herman Kapufi amesema kuwa hatawaandikia barua GGM wasipitishe magari kwaajili ya usalama na pia hatatoa taarifa kwa mkuu wa mkoa juu ya mgogoro uliopo kwenye halmashauri hizo. 

Kwa upanda wake Meneja mwandamizi wa mahusiano kwenye mgodi huo Manase Ndoloma ,amesema kwa upande wao wanaheshimu mabaraza yote mawili na kwamba kwa swala la hilo surusheni yake ni mahakamni  na kwamba wapo tayari kwenda mahakamni kwani ndio chombo pekee ambacho kinatoa haki .
 
Utekelezwaji wa agizo hilo unatarajia kuanza kesho muda wa saa sita za usiku kwa kuzuhia magari kuingia kwenye halmashauri zote mbili na bomba ambalo lipo Rungwe kufungwa.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

No comments